// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); BILA ADEBAYOR SIDHANI KAMA NINGEKUWA VAN MABAO, ASEMA ROBIN VAN PERSIE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE BILA ADEBAYOR SIDHANI KAMA NINGEKUWA VAN MABAO, ASEMA ROBIN VAN PERSIE - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, April 03, 2012

    BILA ADEBAYOR SIDHANI KAMA NINGEKUWA VAN MABAO, ASEMA ROBIN VAN PERSIE

    Van Persie akishangilia moja ya mabao yake
    NI ukweli usiopingika kwamba Robin van Persie ni mmoja kati ya washambuliaji wazuri wa kati – lakini ukweli ni kwamba hakutarajia kutangaza jina lake kupitia nafasi hiyo katika soka.
    Nahodha huyo wa Arsenal, alichukuliwa kama mtu halisi wa kufuata nyayo za Dennis Bergkamp wakati anasaini The Gunners mwaka 2004 na kwa sababu hiyo akapewa jezi namba Namba 10 mwanzoni mwa msimu uliopita.
    Akiwa fiti kabisa ndani ya Arsenal, Van Persie amefunga mabao 54 kwenye mashindano yote, tangu mwanzo wa msimu wa 2011.
    Siri ya mafanikio yake ni kipaji chake, kujituma kuanzia mazoezini, ushauri mzuri na kuwa na malengo ya kufikia kiwango fulani cha ubora kiuchezaji.
    “Nilitumai kucheza kama mshasmbuliaji wa pili... sikuwahi kufikia ningekuwa mshambuliaji wa kwanza,” alisema Van Persie. "Hii tulijaribu tu [akiwa Arsenal] wakati Adebayor alipokwenda Manchester City [mwaka 2009].
    "Kocha hakununua mshambuliaji mwingine pia, kwa sababu alishawishika ningeweza kufanya kazi hiyo, lakini sikushawishika kuamini ningeweza. Sikuwahi kucheza sana katika nafasi hiyo, na sikuwahi kufikiria sana juu ya hiyo kabla.
    "Kocha akasema, 'Nafikiri unaweza kufanya hivi, jitoe, nenda na tuone mwishowake. Cheza mchezo wako wa kawaida, usiende kufunga, nenda kajifurahishe nafsi yako na kuisaidia timu'.
    “Nikaenda na kisha katika kujiandaa na msimu mpya tulikuwa na mechi na Inter Milan na nikafunga bao na kucheza vizuri, na akaniambia baada ya mchezo, 'Tutaona jinsi itakavyoendelea, nina uhakika kwa asilimia 100 itafanya kazi'.
    "Kisha katika mechi zangu tano au sita za kwanza [za ligi] sikufunga, nilikuwa natoa pasi za mabao tu na kucheza vizuri, lakini sikufunga na ninafikiri, 'Mimi ni mshambuliaji wa kwanza sasa, nahitaji kufunga na kocha anasema, 'Sijali hilo, ili mradi unacheza vizuri kwenye timu, unatoa pasi za mabao, mabao yatakuja'.
    "Wakati nafunga bao langu la kwanza, kisha nikafunga mabao saba katika mechi saba, na kutoa pasi za mabao saba, hivyo hiyo ilikuwa nzuri kabisa. Hiyo ndio ilikuwa hatua ya kwanza kuwa mshambuliaji wa kwanza.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: BILA ADEBAYOR SIDHANI KAMA NINGEKUWA VAN MABAO, ASEMA ROBIN VAN PERSIE Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top