Masiello |
BEKI wa Atalanta, Andrea Masiello amekamatawa baada ya taarifa
kwamba alihusika na upangaji wa matokeo na wachezaji wenzake wanane wa zamani
wa Bari na suala lao lipo chini ya uchunguzi, Shirikisho la Soka Italia
limesema leo.
Shirikisho hilo limesema kwamba upangaji wa matokeo
unazorotesha maendeleo ya soka nchini humo na wameahidi kuchukua hatua kwa
atakayekutwa na hatia.Tangu kundi la kwanza la watu 16 wakamatwe Juni, mwaka jana, watu wengine 30 wamekamatwa, akiwemo Nahodha wa zamani wa Atalanta, Cristiano Doni na Nahodha wa zamani wa Lazio, Giuseppe Signori.
Mechi tisa za mwisho za Bari msimu uliopita zinachunguzwa, kwa mujibu wa shirikisho, ikiwemo mechi ambayo bao la kujifunga la Masiello liliisaidia Lecce kushinda 2-0 na kuepuka kushuka daraja, baada ya Bari kuwa tayari imeshuka.
0 comments:
Post a Comment