Drake na Balotelli wakijilia vyao Club |
NYOTA
wa Manchester City, Mario Balotelli amepata rafiki mpya, ambaye bwana wa zamani
wa Rihanna, Drake.
Mario,
ambaye ni shabiki mkubwa wa Hip-hop alimkaribisha rapa huyo mwenye umri wa 25
ambaye alikula raha na Rih mwaka 2009, kuangalia mechi yao na Sunderland Jumamosi.Baada ya mechi hiyo iliyoisha kwa sare ya 3-3, Mario aliamua kumtembeza katikati ya Jiji Drake.
Drake alilipa fadhila kwa Mario walipokuwa MEN Arena Jumapili akimtambulisha kama "memba mpya wa famili lao ".
Aliuambia umati: "Haijalishi yuko timu gani, ni mwanasoka babu kubwa."
Mario alimruhusu Drake kukaa kwenye nafasi yake ya maalum kwenye Uwanja Etihad kushuhudia mchezo huo.
Na Drake baadaye akabandika picha kwenye ukurasa wake wa Facebook chini ya kichwa; Sisi Biashara, ikimuonyeasha amekaa uwanjani amevaa jaketi la City.
Kocha wa City, Roberto Mancini, ambaye hivi karibuni alisema hamuamini Balotelli, atafurahi kusikia mchezaji huyo yuko mbali na Drake baada ya kujirusha Bijou Club, katika usiku ambao nyota wa Coronation Street, Ryan Thomas mchezaji wa QPR, Shaun Wright-Philips walihudhuria.
Bosi wa Bijou, Damien Matto alisema Drake anaipenda club hiyo kwa sababu ina mambo mazuri na ni babu kubwa.
0 comments:
Post a Comment