Wachezaji wa Azam, Said Mourad na John 'Mabao' Bocco 'Adebayor' |
OFISA wa Azam FC, Patrick Kahemele ameandika kwenye ukurasa
wake Facebook kuelezea nia ya klabu hiyo kuutaka ubingwa wa Ligi Kuu, wanaogombea
kwa pamoja na Simba SC.
SOMA:
“Tatizo timu za Tanzania kama walivyo mashabiki wake ni
Simba & Yanga, wachezaji, makocha, viongozi hadi mashabiki wao wamekalia
uwakala wa kuzisaidia Simba na Yanga. Kama Azam FC ingekuwa inashika nafasi ya
saba (7) ikiwa pointi 15 nyuma ya Simba na Yanga msingesikia refa kupigwa wala
nini lakini kwa kuwa kwenye mechi za Azam FC zinaamua nafasi ya Simba/Yanga
kwenye ubingwa na uwakilishi wa nchi kimataifa basi unashangaa watu wanakuja
kuhakikisha wanaisimamisha Azam FC ili wawafurahishe Simba au Yanga.... Tanzania
ni nchi ambayo viongozi wa vilabu vya ligi kuu ni wanachama wa Simba/Yanga tena
wanahudhuria mikutano na kupiga kura, ...... hawa watu wanakuja viwanjani na
chuki, jazba na unazi. Tanzania ni nchi ambayo timu zipo tayari kushuka hata
daraja lakini wawe wametimiza azma yao ya kuzisaidia Simba/Yanga. ni kipindi
cha mpito na kitapita, ndiyo maana tunapigania mpira wetu uwe kwenye TV ili
mambo yanayofanyika kila mtu aone. Azam FC haikatishwi tamaa na itaendelea
kupambana na dhamira yetu ni kuhakikisha tunaleta kikombe cha Afrika in the
next five years.
Waliwatisha na baadaye kuwashusha daraja baadhi ya timu
ambazo zilikuwa zinaleta Challenge, wamejaribu kwa Azam FC wameshindwa na
hakika hawataweza kamwe. Hii ni nchi ambayo mashabiki wake walishangilia Moro
United ya Balhabou kuukosa ubingwa wakati ilikuwa ikiongoza kwa pointi 13 huku
ligi ikiwa imebakiza mechi 5 tuu.... leo walitaka Azam FC ifungwe mfululizo ili
Simba na Yanga zipate nafasi, Tunasema tutapambana hadi mwisho wa ligi... na
Ubingwa Tunautaka,”AMEMALIZA.
0 comments:
Post a Comment