Kikosi cha kwanza cha Simba SC |
Makala Simba hakuna lisilowezekana Imeandikwa na Clecence Kunambi; Tarehe: 27th April 2012 @ 14:30 Imesomwa na watu: 67; Jumla ya maoni: 0 |
ya tatu ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF). Mpaka kufikia hatua hiyo Simba imeziondoa mashindanoni timu za Kiyovu ya Rwanda na Entente Setif ya Algeria na kesho inacheza dhidi ya timu hiyo kutoka Sudan na kama itaiondoa mashindanoni itabakiwa na raundi moja kuingia kwenye makundi. Al Ahly Shandy sio miongoni mwa timu mbili kubwa za Sudan lakini uwepo wa timu hiyo kwenye mashindano hayo sio kitu cha kubeza, kwani ni bora na ndio maana ipo na imefikia hatua hiyo ya mashindano hayo. Simba imekuwa ikicheza vizuri na kwa mbinu kubwa kwenye hatua zote za mashindano hayo, ukianzia mechi ya kwanza dhidi ya Kiyovu mpaka iliyopita dhidi ya Setif na kutokana na kuimarika vizuri kwa timu hiyo kiufundi na kimbinu ndio maana imefika hapo ilipo. Ilianza ugenini dhidi ya Kiyovu ikafanikiwa kupata bao la ugenini katika sare ya bao 1-1 pale Kigali Rwanda, Simba walitangulia kufunga kwa bao la Mwinyi Kazimoto na Wanyarwanda hao kusawazisha. Kwa kanuni za CAF bao moja la ugenini huhesabiwa kama mabao mawili hivyo ni kamaSimba ilishinda kwa mabao 2-1 Kigali na kuhitaji sare ama ushindi wa aina yoyote kusonga mbele. Waliporudiana na timu hiyo kwenye Uwanja wa Taifa Simba chini ya kocha Milovan Cirkovic haikutaka kucheza kwa kutafuta sare bali kupata mabao ya haraka haraka yatakayoihakikishia kusonga mbele, ikafunga mabao mawili ya haraka haraka na hata jamaa wa Kiyovu walipokumbuka shuka kwa bao moja la dakika za mwisho kulikuwa kulishakucha. Kwa staili hiyo ikavuka na safari hii ikapangwa kuanzia nyumbani dhidi ya timu hiyo kutoka Algeria, ambayo nayo ilijitahidi kucheza soka la ugenini kwa kumsimamisha mshambuliaji mmoja mbele na kujaza viungo wengi katikati ya uwanja. Mfumo huo ulionekana kuichanganya sana Simba hasa kipindi cha kwanza kwani walienda mapumziko wakiwa hawajafungana, lakini kikosi hicho Milovan kilibadilika kipindi cha pili kwa kucheza mpira wa kasi huku ikiwatumia vyema wachezaji wake wenye kasi Emmanuel Okwi na Salumu Machaku kuufungua msitu wa waarabu uliojazana golini kwao. Ndipo wakapata mabao mawili ya Haruna Moshi na Okwi lakini huku ikicheza kwa tahadhari kubwa kuizuia Setif isipate hata bao, kwani baada ya Simba kupata mabao yao mawili Setif waliacha mbinu zao chafu za kupaki basi na kuamua kucheza mpira. Na walipokwenda Algeria mbali na kucheza pungufu kwa muda mrefu baada ya beki Juma Nyosso kuoneshwa kadi nyekundu bado walijituma na kutoruhusu zaidi ya mabao matatu na kwa kufanya mashambulizi ya kushtukiza na kutumia uwezo binafsi wa Okwi wakapata bao lililowavusha kwenye hatua hii. Ukifuatilia Simba kwa sasa mbali na uwezo wa wachezaji kama Okwi, Haruna Moshi na Patrick Mafisango kuonekana wa kipekee kutokana na vipaji walivyojaliwa nyota hao na Mwenyezi Mungu lakini wachezaji wengine wote wa ndani ni wa kawaida ila waliounganishwa vyema kitimu. Simba inacheza kitimu sana na inapata mabao yake kwa mfumo unaoeleweka kwa lugha ya soka unaweza kuita mabao ya ‘Move’ yanayotengenezwa vizuri na mawinga wa timu hiyo Okwi, Uhuru Selemani ama Salumu Machaku, ambao wanapokea mipira toka kwa viungo wake Haruna Moshi, Patrick Mafisango na Mwinyi Kazimoto. Kinachopaswa kufanywa na wekundu hao wa Msimbazi ni kama walichofanya katika mechi dhidi ya Setif kutafuta mabao mengi kwa kadiri itakavyowezekana kwenye mechi ya kesho ili wawe na wakati mzuri kwenye mechi ya marudiano huko Sudan. Al Ahly Shandy sio timu ya kubeza kwani inaundwa na nyota wengi waliokuwa wakisugua benchi kwenye timu za El Hilal na El Merreikh, hivyo ni wazi uzoefu walioupata kutoka kwa miamba hiyo kihistoria ya Sudan unaweza ukaisumbua Simba kama wasipokuwa makini. Wacheze soka la kasi na kutumia kila nafasi yatakayoipata huku wakitilia maanani kuwa kwenye mechi za kimataifa huwa hazipatikana nafasi nyingi sana kutokana na umakini wa timu zenyewe, wakishindwa kuzitumia lazima wajue kuwa itawagharimu. Kitu kingine ni kuwa na nidhamu kubwa muda wote wa mechi hiyo waepuke kufanya makosa yatakayowafanya wapate kadi nyekundu hao hata za njano zitakazowafanya kukosa mchezo wa marudiano kwani timu kutoka Uarabuni huwa zinacheza sana na marefa. Hakuna sababu labda mtu fulani awaambie hivyo wao wenyewe kwani wengi wao ni wachezaji wa kimataifa wanafahamu fika gharama za kucheza wakiwa pungufu uwanjani, hivyo nidhamu inapaswa kuwa ya hali ya juu. |
0 comments:
Post a Comment