// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ALONSO AIWANGIA BARCELONA KWA CHELSEA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ALONSO AIWANGIA BARCELONA KWA CHELSEA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, April 23, 2012

    ALONSO AIWANGIA BARCELONA KWA CHELSEA


    Xabi Alonso - Real Madrid
    Xabi Alonso - Real Madrid
    KIUNGO wa Real MadridXabi Alonso ameihakikishia Chelsea kwamba Barcelona si timu isiyofungika kwenye Uwanja wake wa Camp Nou.

    The Blues ina kipaumbele cha bao dhidi ya klabu hiyo ya Katalunya ikijiandaa kumenyana nayo katika mechi ya marudiano ya Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa kesho, na Alonso, mmoja wachezaji wa Real Madrid walioifunga timu hiyo ya  Pep Guardiola katika  El Clasico Jumamosi , anaamini kwamba licha ya vipaji vyao, mabingwa hapo watetezi wanafungika.

    "Sababu hiyo haitokani na leo tu," alisema Alonso . "Lakini siku nyingine pia. Tuliona Chelsea wakiwafunga.

    "Tunafahamu kwamba miaka michache iliyopita, Barcelona wamekuwa na mafanikio ile mbaya, kwamba walikuwa wakicheza babu kubwa, soka ya kustaajabisha. Lakini wao si timu isiyofungika.

    "Chelsea wanaongoza. Wako mbele katika mabao. Kucheza hapa ni vigumu, lakini tutaona kitakachotokea."alisema.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ALONSO AIWANGIA BARCELONA KWA CHELSEA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top