Ferguson |
Mzaliwa huyo wa Beirut mwaka 1957, Mr Midani alijiunga na klabu hiyo ya Old Trafford mwaka 1987 wakati United ilipoinunua klabu ya mpira wa kikapu ya Manchester Giants, ambayo alikuwa Mwenyekiti wake.
Awali alikuwa raia wa Lebanon na bingwa wa michuano ya watoto ya table tennis akiwa ana umri wa miaka 15 na alihamia England akiwa ana umri wa miaka 18.
“Nilistaajabishwa sana kusikia habari hizo, kwa sababu umri wa miaka 55 si mkubwa,” alisema rais wa heshima wa United, Martin Edwards.
“Tulimfahamu alipojiunga na bodi na wakati wote alikuwa mtu safi na alikuwa anapendwa sana Old Trafford. Kwa kiasi kikubwa na habari za kuhuzunisha na daima atakumbukwa na kila mmoja aliyemtambua.”
Sir Alex Ferguson, kuchaguliwa kocha wa klabu hiyo ni miongoni mwa maamuzi yaliyochukuliwa na bodi ya United baada ya kuwasili kwa Mr Midani:
"Aliunga mkono sana kuajiriwa kwangu na wakati wote nakubali juu ya uelewa wake kwa kazi yangu Old Trafford,”alisema Fergie"
Kila mtu katika klabu ya Manchester United angependa kutoa pole kwa familia ya Mr Midani.
0 comments:
Post a Comment