Adebayor kushoto |
MSHAMBULIAJI Emmanuel Adebayor alipiga mabao mawili wakati
Tottenham ikiifunga Swansea 3-1 leo na kuifikia kwa pointi Arsenal katika mbio
za kuwania nafasi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mshambuliaji huyo wa Togo alifunga mabao hayo dakika za 73
na 87 na kufikisha mabao 13 na kuzima jinamizi la Spurs kutoshinda mechi tano
kwenye Ligi Kuu.
Zikiwa zimebaki mechi saba, Tottenham iko nyuma ya Arsenal kwa
tofauti ya mabao tu na inazizidi pointi tano dhidi ya Chelsea na Newcastle.
Kiungo wa Uholanzi, Rafael van der Vaart aliifungia Spurs
bao la kuongoza kwenye Uwanja wa White Hart Lane dakika ya 19, kabla ya Gylfi
Sigurdsson kusawazisha karibia dakika ya 60.
0 comments:
Post a Comment