Nditi mwenye kasi uwanjani na mpishi mzuri wa mabao kwa krosi zake, amekwishaichezea timu ya vijana ya Chelsea mechi 27 na kwa sasa panga pangua hakosekani kwenye 11 wa kuanza.
Lakini mchezaji huyo hawezi kuchezea timu yoyote ya taifa ya Tanzania kwa sababu ya sheria ngumu ya nchi hii, kumzuia raia wake kuwa na uraia wa pili.
Nchi nyingi Afrika, zinaruhusu raia wake kuwa na uraia wa pili na wachezaji wengi wakubwa wa Afrika kama akina Didier Drogba, Yaya Toure, Asamoah Gyan, Saydou Keita, Dennis Oliech, McDonald Mariga, pamoja na uraia wa nchi zao, wana uraia wa Ulaya pia.
Lakini pamoja na kuwa na uraia wa Ulaya, mwisho wa siku wanapostaafu soka hurejea Afrika kuzisaidia nchi zao, mfano wachezaji waliostaafu siku za karibuni kama Celestine Babayaro wa Nigeria, Rogobert Song wa Cameroon wote wanafanya kazi ya soka nchini mwao.
Huwezi kumuacha Mwafrika pekee aliyetwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, George Weah ambaye amejiingiza hadi kwenye siasa akitaka kuwa mwanasoka wa kwanza mkubwa duniani kuwa rais wan chi duniani.
Weah alipostaafu alikuwa akiifadhili timu ya taifa ya Liberia na hata sasa akiwa ana ndoto za kuwa rais wa nchi hiyo, moja ya mikakati yake ni kuifanya nchi hiyo iwe tishio kwenye soka.
Endapo sheria hii haitabadilishwa Tanzania, Nditi anayeendelea vizuri anaweza kuamua kuchezea England kwa sababu kwa soka yake haitashangaza siku moja akiitwa timu ya taifa, ikiwa anang’ara klabu kubwa kama Chelsea na amekwishatwaa nayo ubingwa wa Kombe la FA la vijana.
Mwaka 2006, Kali Ongala anayezaliwa na baba Mtanzania mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) marehemu Dk Remmy Ongala na mama Muingereza, alishindwa kuichezea timu ya taifa, licha ya kuhitajiwa sana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbrazil, Marcio Maximo.
Wakati huo akichezea Vasby United ya Sweden, Kali alikuwa yupo katika kiwango kizuri na dhahiri kukosekana kwake kulipunguza nguvu ya kikosi ambacho mwishowe kilikosa tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2008 Ghana.
Mshambuliaji wa kikosi hicho alikuwa Gaudence Mwaikimba wakati Kali, ambaye kwa sasa ni kocha Msaidizi wa Azam FC akishindwa kutimiza ndoto zake za kuchezea nchi ambayo ana mapenzi nayo na iliyomuinua kisoka akianzia Abajalo ya Sinza, baadaye Yanga kabla ya kwenda Marekani, England, Jamaica na kumalizia soka yake Sweden. Mnasemaje wadau. Maoni yenu.
Adam Nditi |
KATIKA tovuti ya Chelsea (chini kulia), wameandika kuwa
kiungo chipukizi Mtanzania, Adam Nditi anayechezea timu ya vijana ya klabu
hiyo, anacheza kama beki wa kimataifa wa England, Ashley Cole.
Nditi aliyezaliwa Septemba 18, mwaka 1994 visiwani Zanzibar,
Tanzania, alitua Chelsea na kuanzia katika kikosi cha vijana chini ya umri wa
13, akicheza nafasi za beki ya kushoto na winga ya kushoto.Nditi mwenye kasi uwanjani na mpishi mzuri wa mabao kwa krosi zake, amekwishaichezea timu ya vijana ya Chelsea mechi 27 na kwa sasa panga pangua hakosekani kwenye 11 wa kuanza.
Lakini mchezaji huyo hawezi kuchezea timu yoyote ya taifa ya Tanzania kwa sababu ya sheria ngumu ya nchi hii, kumzuia raia wake kuwa na uraia wa pili.
Nchi nyingi Afrika, zinaruhusu raia wake kuwa na uraia wa pili na wachezaji wengi wakubwa wa Afrika kama akina Didier Drogba, Yaya Toure, Asamoah Gyan, Saydou Keita, Dennis Oliech, McDonald Mariga, pamoja na uraia wa nchi zao, wana uraia wa Ulaya pia.
Lakini pamoja na kuwa na uraia wa Ulaya, mwisho wa siku wanapostaafu soka hurejea Afrika kuzisaidia nchi zao, mfano wachezaji waliostaafu siku za karibuni kama Celestine Babayaro wa Nigeria, Rogobert Song wa Cameroon wote wanafanya kazi ya soka nchini mwao.
Huwezi kumuacha Mwafrika pekee aliyetwaa tuzo ya Mwanasoka Bora wa Dunia, George Weah ambaye amejiingiza hadi kwenye siasa akitaka kuwa mwanasoka wa kwanza mkubwa duniani kuwa rais wan chi duniani.
Weah alipostaafu alikuwa akiifadhili timu ya taifa ya Liberia na hata sasa akiwa ana ndoto za kuwa rais wa nchi hiyo, moja ya mikakati yake ni kuifanya nchi hiyo iwe tishio kwenye soka.
Endapo sheria hii haitabadilishwa Tanzania, Nditi anayeendelea vizuri anaweza kuamua kuchezea England kwa sababu kwa soka yake haitashangaza siku moja akiitwa timu ya taifa, ikiwa anang’ara klabu kubwa kama Chelsea na amekwishatwaa nayo ubingwa wa Kombe la FA la vijana.
Mwaka 2006, Kali Ongala anayezaliwa na baba Mtanzania mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) marehemu Dk Remmy Ongala na mama Muingereza, alishindwa kuichezea timu ya taifa, licha ya kuhitajiwa sana na aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Mbrazil, Marcio Maximo.
Wakati huo akichezea Vasby United ya Sweden, Kali alikuwa yupo katika kiwango kizuri na dhahiri kukosekana kwake kulipunguza nguvu ya kikosi ambacho mwishowe kilikosa tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2008 Ghana.
Mshambuliaji wa kikosi hicho alikuwa Gaudence Mwaikimba wakati Kali, ambaye kwa sasa ni kocha Msaidizi wa Azam FC akishindwa kutimiza ndoto zake za kuchezea nchi ambayo ana mapenzi nayo na iliyomuinua kisoka akianzia Abajalo ya Sinza, baadaye Yanga kabla ya kwenda Marekani, England, Jamaica na kumalizia soka yake Sweden. Mnasemaje wadau. Maoni yenu.
0 comments:
Post a Comment