Ibra |
AC Milan iliruhusu nyavu zake kutikiswa
dakika ya 90 na mshambuliaji wa Fiorentina, Amauri hivyo kujikuta ikilala 2-1 nyumbani
leo na kujiongezea maumivu baada ya kutolewa na Barcelona kwenye Ligi ya
Mabingwa Ulaya, siku nne zilizopita.
Kipigo hicho kinaifanya Milan ibaki
inaizidi pointi mbili tu Juventus kileleni mwa Serie A, na wanawapa Kibibi
Kizee cha Turin nafasi ya kuongzoa ligi iwapo wataifunga Palermo baadaye.
Milan ilipata bao la kuongoza
kwa mkwaju wa penalti wa Zlatan Ibrahimovic dakika ya 31 kwenye Uwanja wa San
Siro, lakini Stevan Jovetic akasawazisha dakika ya 47.
Nayo Inter Milan imetoka sare ya
2-2 na Cagliari iliyomaliza mechi na wachezaji 10, hiyo ikiwa mechi ya pili
chini ya kocha wao mpya, Andrea Stramaccioni.
Katika mechi hiyo iliyocheza
huko Trieste, kwa sababu ya mgogoro wa Cagliari na Halmashauri ya Jiji lao juu
ya ukarabati wa Uwanja wa Sant’Elia, Davide Astori aliifungia bao la kuongoza Cagliari
kwa tik tak dakika ya tano na Diego Milito akasawazisha dakika moja baadaye.
Mshambuliaji wa Chile, Mauricio
Pinilla aliifungia la pili Cagliari dakika ya 61 kisha akaonyeshwa kwa
ushangiliaji wake na Esteban Cambiasso akasawazishia Inter tena dakika tatu
baadaye.
Nayo, Udinese iliifunga Parma
3-1 na kuifikia Lazio katika nafasi ya tatu. Mshambuliaji wa Ghana, Kwadwo
Asamoah alifunga mabao mawili kwa Udinese na Antonio Di Natale pia alifunga bao
lake la 20 msimu huu.
Lazio inamenyana na Napoli inayoshika
nafasi ya tano baadaye.
Roma imefungwa 4-2 na Lecce, Chievo
Verona imeifunga Catania 3-2; Bologna imetoka 0-0 na Cesena; na Novara imetoka
1-1 na Genoa.
Mechi zote 10 za Ligi ya Italia
zinachezwa leo kwa sababu kesho ni sikukuu ya Pasaka.
0 comments:
Post a Comment