// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA NA AFRICAN LYON DAR, SIMBA NA POLISI DOM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA NA AFRICAN LYON DAR, SIMBA NA POLISI DOM - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 14, 2012

    YANGA NA AFRICAN LYON DAR, SIMBA NA POLISI DOM


    Kikosi cha Yanga 
    TIMU za Simba na Yanga za Dar es Salaam leo zinaingia kwenye viwanja tofauti katika mfululizo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, baada ya mwishoni mwa wiki kushindwa kung’ara.
    Yanga itaingia Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza na African Lyon ikijaribu kujisafisha baada ya Jumamosi kufungwa mabao 3-1 na Azam kwenye uwanja huohuo, huku Simba ikiwa ugenini Uwanja wa Jamhuri, Dodoma kuivaa Polisi ya mjini humo.
    Yanga inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 37 kwa michezo 19, huku Azam ikishika nafasi ya pili ikiwa na pointi 41 sawa na Simba inayoongoza ligi hiyo ikiwa pia na pointi 41, lakini ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga.
    Mchezo wa Yanga na African Lyon unatarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kutokana na Yanga kuwa na hasira ya kufungwa na Azam, hivyo itataka ishinde ikae sawa kwenye msimamo wa ligi.
    Lakini Lyon nayo haipo pazuri kwenye msimamo wa ligi, ikiwa nafasi ya kumi kwenye msimamo kati ya timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo baada ya kujikusanyia pointi 18 kwa michezo 18.
    Hivyo ni wazi mchezo huo utakuwa wa vuta nikuvute kwani Lyon sasa itakuwa inapigania kutoka kwenye ukanda wa kushuka daraja, huku Yanga ikipambana kuhakikisha inapunguza pengo lake la pointi na vinara wa ligi hiyo.
    Kwa upande wa Simba baada ya Jumapili kutoka 0-0 na Toto Africans ya Mwanza inayoshika nafasi ya pili kutoka mkiani, leo itacheza na Polisi inayoshika nafasi ya mwisho mkiani.
    Lakini Polisi licha ya kuburuza mkia ikiwa na pointi 14 kwa michezo 19, imekuwa ikiisumbua Simba mara kwa mara zinapokutana, hivyo ni wazi mchezo wa leo utakuwa na ushindani wa aina yake.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA NA AFRICAN LYON DAR, SIMBA NA POLISI DOM Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top