// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); YANGA, AZAM MECHI LA KIMATAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE YANGA, AZAM MECHI LA KIMATAIFA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 06, 2012

    YANGA, AZAM MECHI LA KIMATAIFA


    Kikosi cha Yanga kilichotoa sare ya 1-1 na Zamalek 

    KUNA mechi nyingine katika Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara zina mvuto wa michuano ya Afrika, kama Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa michuano ambayo Yanga wametolewa na Zamalek mwishoni mwa wiki.
    Bila shaka, hata mechi kati ya Azam FC na Yanga Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam inaweza kuwa tamu pengine kuliko hata ile mechi ya Simba na Kiyovu.
    Yanga inashuka dimbani kwenye Uwanja wa Taifa Jumamosi kumenyana na Azam, ikiwa ina hasira nao ile mbaya.
    Hasira za Yanga zinatokana na nini? Kwanza wamefungwa na Zamalek na kutolewa kwenye michuano ya Afrika mapema kama ilivyo kawaida yao.
    Lakini pili, Yanga imefungwa na Azam mara mbili mfululizo- kwanza kwenye mechi ya Ligi Kuu 1-0 kwenye Ligi Kuu Septemba 18, mwaka jana Uwanja wa Taifa na baadaye kwenye Kombe la Mapinduzi Januari, mwaka huu.
    Lakini yote tisa, 10 ni kwamba Yanga inataka kupoza machungu ya mashabiki wake baada ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa- hivyo Jumamosi watataka kushinda kwa lazima, licha ya ubora wa Azam wanoutambua.       
    Yanga iliyorejea Jumatatu kutoka Cairo, inasifiwa kucheza soka ya kuvutia licha ya kufungwa na Zamalek, jambo ambalo linawafanya mashabiki wa timu hiyom wawe na hamu kubwa ya kuiona timu yao.
    Mechi ya Jumamosi itawakutanisha vinara wa mabao katika Ligi Kuu, John Bocco kwa upande wa Azam anayeongoza kwa mabao yake 12 na Kenneth Asamoah kwa Yanga, anayefuatia kwa mabao yake 10.
    Lakini pia itawakutanisha makipa wanaowania kumvua glavu Juma Kaseja katika timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Mwadini Ally wa Azam na Shaaban Kado wa Yanga ambao wote ni makipa wa akiba katika kikosi cha Mdenmark Jan Borge Poulsen.
    Haruna Hakizimana Fadhil Niyonzima kwa sasa unaweza kusema ndiye mchezaji bora zaidi wa kigeni katika Ligi Kuu- lakini Azam pia ina viungo wazuri wazawa kama Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Abdi Kassim ‘Babbi’ na Jabir Aziz, ambao wote wanaifanya mechi hiyo iwe na ‘quality’ za Afrika.
    Kocha Muingereza Stewart Hall, baada ya kutwaa Kombe la Mapinduzi Januari mwaka huu, katika michuano iliyoshirikisha Simba na Yanga, tena akizifunga timu zote hizo, ameweka bayana sasa anataka kufuta utawala wa vigogo hao na kwenye Ligi Kuu ya Bara.
    Lakini kocha aliyekalia kuti kavu Yanga, Mserbia Kostadin Bozidar Papic hatahitaji presha zaidi na dawa ya kuepuka hali hiyo ni ushindi tu Jumamosi.
    Mambo mengine yanayoifanya mechi hiyo iwe tamu ni kwamba Azam ina wachezaji ambao misimu michache iliyopita walikuwa wanang’ara Yanga kama Mrisho Ngassa na Abdi Kassim.   

    REKODI YA YANGA AZAM FC:
    Septemba 18, 2011
    Azam 1-0 Yanga
    Machi 30, 2011
    Yanga 2-1 Azam
    Oktoba 24, 2010
    Azam 0-0 Yanga
    Machi 7, 2010
    Yanga 2-1 Azam          
    Oktoba 17, 2009
    Azam 1-1 Yanga     
    Aprili 8, 2009
    Yanga 2-3 Azam FC 
    Oktoba 15, 2008
    Azam FC 1-3 Yanga
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: YANGA, AZAM MECHI LA KIMATAIFA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top