Wenger |
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amefungiwa mechi tatu na
kutozwa faini ya Euro 40 000 (dola za KImarekani 53,100) kwa kuwavaa marefa
baada ya timu yake kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na AC Milan mwezi huu.
UEAFA imesema jana kwamba Mfaransa huyo alikuwa na hatia kwa
kitendo chake kwenye mechi ya mwisho ya hatua ya 16 bora Ligi ya Mabingwa, Arsenal
ikishinda 3-0 na kutolewa kwa jumla ya mabao 4-3.
Wenger, ambaye awali alifungiwa mechi moja baada ya kwa kosa
kama hilo baada ya kutolewa na Barcelona katika hatua kama hiyo, kasha akasimamishwa
mechi mbili kupuuza adhabu hiyo, amesema atakata rufaa.
Akizungumza juzi na Waandishi wa Habari kabla ya UEFA kutangaza
adhabu hiyo, Wenger alisema: "Kama nitasimamishwa na haitafafanuliwa,
nitakata rufaa moja kwa moja. Naamini kwamba wamewatukuza marefa wa mashindano
ya UEAFA na kuwa wasiogusika, kiasi kwamba huwezi hata kuwaambia neno. Kitu pekee
wanachoelewa baada ya mechi ni taarifa.
"Naamini kwamba kama una miaka 25 mfululizo Ulaya, unaweza
kuendelea kuwauliza marefa kama unaweza kumuuliza kitu. Ni vigumu kuelewa."
0 comments:
Post a Comment