// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WATANZANIA KUAMUA AC LEOPARDS V CLUB SPORTIF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WATANZANIA KUAMUA AC LEOPARDS V CLUB SPORTIF - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, March 16, 2012

    WATANZANIA KUAMUA AC LEOPARDS V CLUB SPORTIF


    Mwamuzi Waziri Sheha wa Tanzania ameteuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kuchezesha mechi namba 51 ya Kombe la Shirikisho kati ya AC Leopards ya Jamhuri ya Congo na Club Sportif Sfaxien ya Tunisia.

    Katika mechi hiyo itakayochezwa jijini Brazzaville kati ya Machi 23, 24 na 25 mwaka huu, Sheha atasaidiwa na waamuzi John Kanyenye na Ferdinand Chacha wakati mezani atakuwa Ramadhan Ibada. Waamuzi wote hao wasaidizi pia wanatoka Tanzania. Kamishna atakuwa Zeli Sinko kutoka Ivory Coast.

    Naye Hafidh Ally wa Tanzania ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi namba 53 ya Kombe la Shirikisho kati ya Lydia LB Academic ya Burundi na Enppi ya Misri itakayochezwa jijini Bujumbura kati ya Machi 23, 24 na 25 mwaka huu
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WATANZANIA KUAMUA AC LEOPARDS V CLUB SPORTIF Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top