Mabango ya chama cha wachezaji Uganda, vipi SPUTANZA ya bongo, inatetea haki za wachezaji ipasavyo? |
MECHI za Ligi Kuu ya Uganda, (USL) wiki hii zimesimamishwa
ili kutoa fursa kwa wachezaji na klabu kueleza matatizo yao.
Katika Mkutano uliohudhuriwa na viongozi wa klabu 13 kati ya
jana jioni, wawakilishi wa Victors, Ivan Bagyenda, KCC John Mutenda na Express,
Kavuma Kabenge pia waliteuliwa kuongoza mazungumzo kati ya klabu na chama cha
wachezaji.
Chama cha Shirikisho la Wachezaji (Fofpa), kinachowakilisha
wachezaji, walianza mgomo Ijumaa iliyopita wakitaka waboreshewe mambo kadhaa na
Shirikisho la Soka Uganda (Fufa), ikiwemo maslahi.
“Tumeamua kusimamisha mechi za Jumanne, Ijumaana Jumamosi za
USL kutoa fursa kwa klabu na wachezaji kuwasilisha matatizo yao,” alisema Kabenge,
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kampuni ya Ligi Kuu, USL baada ya kikao cha jana
katika hoteli ya Sheraton Hotel, Kampala.
Mechi zilizotarajiwa kupigwa leo ni kati ya Bidco vs Maroons
na Hoima-Busia vs URA. Mechi sita zaidi zilitarajiwa kupigwa Ijumaa na Jumamosi.
Kikao
hicho kilifungua dirisha la dharula la usajili kwa siku saba kuanzia leo, ili
kutoa fursa kwa klabu kusajili na wachezaji kuhama. Ligi Kuu inatarajiwa kuendelea
tena Jumanne inayo
0 comments:
Post a Comment