// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WACHEZAJI UGANDA WASUSIA LIGI KUU, FUFA INALO HILO! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WACHEZAJI UGANDA WASUSIA LIGI KUU, FUFA INALO HILO! - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 10, 2012

    WACHEZAJI UGANDA WASUSIA LIGI KUU, FUFA INALO HILO!


    Yassin Mugabi

    MGOMO wa wachezaji katika Ligi Kuu ya Uganda , Bell Super League umeingia katika siku ya pili leo, safari hii ukihusisha mechi kati ya Proline na Water kwenye Uwanja wa Nakivubo jioni ya leo.
    Wachezaji wa Ligi Kuu wametupa taulo zao Ijumaa wakitoa madai kadhaa ikiwemo kulalamikia mfumo mzia wa Shirikisho la Soka Uganda (FUFA), viwango vya mikataba na haki zao, jambo ambalo limesababisha mechi tatu kutochezwa ndani ya siku mbili.
    Kama ilivyokuwa katika mechi ya Bombo ambako Simba ilikipiga na Express jana, ilibidi isimamishwe baada ya wachezaji saba wa Red Eagles kushindwa kuendelea na mchezo kwa madai ni majeruhi, Water pia ilianza na wachezaji saba dhidi ya 11 wa Proline, baada yaw engine kutotokea.
    Dajkikam tisa ndani ya mchezo huo, Kasule Umar naye akaanguka chini kwa majeruhi. Alitibiwa na watu wa huduma ya kwanza ili kurejea uwanjani, lakini ikashindikana, huku akipigiwa makofi na watoto wa shule katika mechi iliyohezwa kwenye Uwanja ‘mweupee’.
    Kwa mujibu wa sheria za soka, refa alilazimika kuvunja mechi hiyo kutokana na Water kubaki na wachezaji sita tu.
    Watu wengine walisema Umar alidanganya kuumia, lakini kocha wake, Charles Ayiekoh alimtetea.
    “Si kweli,” alisema Ayiekoh na kuongeza; “Amekuwa akisumbuliwa na tatizo la goti na alikosa mechi zetu mbili zilizopita,”alisema.
    “Hivyo nilipofika hapa na kukuta wachezaji sita tu wamefika kwa ajili ya mechi, ikabidi nimpigie simu yeye aje. Inauma, maunmivu yamemrudia.”
    Wakati Umar anaanguka, kipa Yasin Mugabi alikuwa amekwishawapa Proline bao la kuongoza dakika ya tatu kwa mpira wa adhabu.
    Mechi nyingine kati ya KCC na Hoima-Busia na Maroons dhidi ya Polisi, puia hazikuendelea.
    Kampuni ya Ligi Kuu Uganda, USL itakutana na klabu za Ligi Kuun Jumatatu kujaribu kutatua tatizo hilo.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WACHEZAJI UGANDA WASUSIA LIGI KUU, FUFA INALO HILO! Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top