WABUNGE 6 akiwemo Menyekiti wa klabu ya Simba, Ismail Rage watakuwepo Setif nchini Algeria kushuhudia mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho kati ya Simba na ES Setif mwishoni mwa wiki ijayo. Akizungumza na gazeti la Habari Leo jana, Rage ambaye pia ni Mbunge wa Tabora Mjini (CCM), aliwataja wabunge wengine wa Tanzania kuwa ni Khalifa Suleiman Khalifa (Gando-CUF), Murtaza Mangungu (Kilwa Kaskazini- CCM) na Zitto Kabwe (Kigoma Kaskazini-Chadema). "Zitto amenieleza ataungana nasi Algeria akitokea Nigeria, pia atakuwepo Hasnain Murji na Mussa Azzan 'Zungu' (Ilala-CCM), ambaye naye atajiunga nasi akitokea Morocco. "Tumejipanga vya kutosha, ninaamini vijana watapata hamasa ya kutosha na mambo yatakuwa mazuri zaidi, tuna matumaini makubwa tutafanya vizuri," alisema Rage. Aliwaomba mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi Jumamosi kwenye mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kati ya Simba na African Lyon ili kuwapa nguvu wachezaji ya kwenda kufanya vizuri Algeria. Alisema Simba inatarajiwa kuondoka Dar es Salaam Jumatatu na italala Cairo, Misri na siku inayofuata itaanza safari ya kwenda Algeria, ambapo wenyeji wao wamewajulisha mchezo utafanyika mji wa Setif. “Kutoka Algiers hadi Setif hapo itakuwa jukumu la wenyeji kutugharamia, maana taratibu za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) zinasema ikizidi Kilometa 200 itabidi usafiri unaotumika uwe wa ndege, sasa kutoka Algiers hadi Setif ni zaidi ya Kilometa 200,” alisema Rage. Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wa kwanza raundi ya kwanza Kombe la Shirikisho dhidi ya ES Seti Jumapili Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, ambapo ili isonge mbele inahitaji ushindi wa aina yoyote, au sare ya aina yoyote ama isifungwe zaidi ya bao 1-0. |
Cody Gakpo urges 'special' Mohamed Salah to stay at Liverpool beyond this
season and insists the Reds are 'very lucky to have him' - with talisman's
contract expiring in the summer
-
Once again Salah has been instrumental to their success, and he recently
became the first Premier League player to have double figures in goals and
assists...
43 minutes ago
0 comments:
Post a Comment