// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); WAALGERIA KUTUA ALHAMISI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE WAALGERIA KUTUA ALHAMISI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 19, 2012

    WAALGERIA KUTUA ALHAMISI

    Abdelmaliek Ziaya mshambuliaji wa  ESS Setif
    WAKATI kikosi cha timu ya soka ya Simba kinatarajiwa kuingia kambini
    leo kujiandaa na mechi yake ya kombe la Shirikisho dhidi ya ES Setif
    ya Algeria, wapinzani wao hao wanatarajiwa kuwasili nchini Alhamisi 
    tayari kwa mchezo huo wa kwanza utakaopigwa jumapili katika dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.
    Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage alisema msafara wa watu 37 kutoka Algeria utafikia katika hoteli ya Durban iliyopo katikati ya jiji la Dar es Salaam. Alisema maandalizi kwa ajili ya mchezo huo yanakwenda vema ambapo kikosi cha Simba kilichopewa mapumziko ya siku moja baada ya kutoka Morogoro ilipocheza na Mtibwa Sugar ya huko na kuchanua na ushindi wa mabao 2-1, kitaingia kambini katika hoteli ya Bamba Beach iliyopo Kigamboni, jijini Dar es Salaam. Rage aliongeza kuwa kikosi chake kipo katika hali nzuri na kwa siku zilizosalia kabla ya mchezo huo anaamini kocha mkuu wa timu hiyo Mserbia Milovan Cirkovic atazitumia vema kukiweka katika hali nzuri zaidi ili kuweza kushinda mechi hiyo. Mechi hiyo itakayopigwa kuanzia saa 10 kamili jioni itachezeshwa na waamuzi kutoka Rwanda ambapo mwamuzi wa kati atakuwa Hudu Munyemana wakati wasaidizi wake ni Felicien Kabanda, Theogene Ndagijimana na Edouard Bahizi. Kamishna wa mechi hiyo ni Felix Tangawarima kutokaZimbabwe. Timu hizo zitarejeana Algeria Aprili 6 na iwapo Simba itashinda itacheza mechi ya kwanza nyumbani Aprili 29 mwaka huu na mshindi kati ya El Ahly Shandy ya Sudan na Ferroviario de Maputo ya Msumbiji ambapo ya marudiano itachezwa kati ya Mei 11, 12 na 13 mwaka huu. Katika hatua nyingine, kiungo wa timu hiyo Rajab Isihaka amefiwa na baba yake mzazi Mzee Isihaka ambaye alikutwa na umauti huo asubuhi ya jana jijini Dar es Salaam ambapo msimba upo nyumbani kwa marehemu Mbagala Mbagala Charambe jijini Dar es Salaam huku mazishi yakitarajiwa kufanyika leo.mwisho
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: WAALGERIA KUTUA ALHAMISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top