// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); VITALI AMGWAYA GEORGE FOREMAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE VITALI AMGWAYA GEORGE FOREMAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, March 16, 2012

    VITALI AMGWAYA GEORGE FOREMAN


    Vitali
    KIEV, Ukraine
    BINGWA wa ndondi uzito wa juu anayetambuliwa na WBC, Vitali Klitschko amesema hana mpango wa kjuvunja rekodi ya George Foreman kutwaa ubingwa wa dunia akiwa mzee zaidi, kwani anatakakuelekeza nguvu zake kwenye siasa nchini mwao Ukraine.
    Alipoulizwa Jumatatu ana muda gani wa kuendelea kutupa masumbwi ulingoni, mbabe huyo mwenye umri wa miaka 40, Klitschko alisema “Si muda mrefu” na kuongeza kwamba “Najielekeza kwenye siasa kwa sababu Ukraine ina hamu kubwa.”
    George Foreman anashikilia rekodi ya bondia mzee zaidi kutwaa ubingwa wa dunia akiwa ana umri wa miaka 45 mwaka 1994, na Klitschko alisema “Sitaki kuvunja rekodi ya George Foreman.”
    Klitschko yuko chama cha upinzani kiitwacho “Udar” (Strike) na anataka kuwa Meya wa Kiev, nafasi ambayo aliikosa mwaka 2006 baada ya kukumbwa na kashfa ya rushwa. Ataingia kwenye hatua za awali za uchaguzi wa jimbo hilo baadaye mwaka huu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VITALI AMGWAYA GEORGE FOREMAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top