// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); VIBABU TATIZO INTER MILAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE VIBABU TATIZO INTER MILAN - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 15, 2012

    VIBABU TATIZO INTER MILAN

    Kocha wa zamanio wa Inter Milan, Mourinho akifuarahia mafanikio na timu yake mpya, Real Madrid. je, lilikuwa kosa kumyuachia Mreno huyo kuondoka? 
    IDADI kubwa ya wachezaji ambao umri umewatupa mkono ndani ya klabu ya Inter Milan ya Iatlia ndio chanzo cha kushuka na kwa Mabingwa hao wa Ulaya  mwaka 2010 hadi kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa na Olympique Marseille ya Ufaransa.
    Rais wa klabu hio Massimo Moratti alimuondolea makosa kocha Claudio Ranieri kufuatia mchuano wa jumanne kutokana na magoli ya ugenini.
    Mchuano huo ulimalizika 2-2 baada ya Inter kushinda nyumbani 2-1, lakini bao la ugenini likabadili matokeo na hivyo kuashiria kua Inter msimu huu inaondoka kapa bila Kombe hata moja.Klabu hio imeisha ondolewa katika mashindano ya Kombe la Italia ikiwa ya saba kwenye msimamo wa Ligi ya Serie A.
    Hali hii ilianza punde baada ya kocha wao Jose Mourinho kuondoka kufuatia ushindi wa makombe matatu miaka miwili iliyopita.
    Mreno huyo mjanja alifahamu vyema umri wa kikosi cha Inter kua hautoiwezesha kufikia kiwango hicho tena na kuondoka na heshima yake.
    Rafa Benitez akafuata kujaribu bahati yake, akashindwa na Leonardo akamrithi naye akianguka, kisha akaja Gian Piero Gasperini na baada ya kushindwa ndio akateuliwa Ranieri.
    Rais wa Inter amesema haifai kufikiria mageuzi bali ni marekebisho.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: VIBABU TATIZO INTER MILAN Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top