KLABU ya Malaga ilitoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya
Espanyol jana na kupanda hadi nafasi ya nne katika Ligi Kuu ya Hispania, hivyo
kufufua matumaini ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.
Mabao ya Malaga yalifungwa na Ruud van Nistelrooy na Martin
Demichelis ndani ya dakika tatu kipindi cha pili, wakati bao la timu
inayomilikiwa na bilionea wa Qatari, lilifungwa na Philippe Coutinho dakika ya 24.Malaga inalingana kwa pointi na Valencia inayoshika nafasi ya tatu na kuwapiku Levante waliopigwa 2-0 na Osasuna, mabao ya Raul Garcia na Juan Francsico Martinez.
Osasuna imepanda nafasi ya sita ambayo wakiikali hadi mwisho watacheza Europa League.
Wakati huo huo: Athletic Bilbao ililazimishwa sare ya 1-1 nyumbani
na Sporting Gijon, ikiwa ni mechi ya nne mfululizo wanacheza bila kushinda
tangu waitoe Manchester United Ulaya.
Athletic ilikuwa ya kwanza kupata bao, mfungaji Oscar de
Marcos kwenye Uwanja wa San Mames dakika ya77, lakini Alberto Lora akasawazisha
dakika ya 90.
0 comments:
Post a Comment