TIMU ya taifa ya Uganda ikicheza na wachezaji pungufu 10, katika mechi yao ya kwanza ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika mwaka 2013 ilikiona cha moto mbele ya Congo Brazzaville baada ya kuchapwa mabao 3-1 mjini Pointe Noire jana.
Henry Kalungi alijifunga mapema dakika ya kwanza kabla ya mkwaju wa penalti wa Lepicier Tsonga na Matt Missilou Massamba kufunga baadaye na kuiweka mbele Red Devils kwa 3-0.
Mike Sserumaga aliifungia Uganda bao muhimu la kufutia machozi na sasa kocha Bobby Williamson atatakiwa kushinda 2-0 kwenye mchezo wa marudiano Juni 15 mjini Kampala ili kusonga mbele.
Tonny Mawejje atakosa mchezo wa marudiano kufuatia kiungo huyo kutolewa nje baada ya kuonyeshwa kadi mbili za njano kwenye mechi hiyo.
0 comments:
Post a Comment