NYON, Uswisi
MECHI kati Barcelona na Real Madrid “Clasico,” Jose Mourinho kukutana tena na Chelsea au
marudio ya fainali ya kwanza, misimu 20 iliyopita baina ya AC Milan na
Marseille ni miongoni mwa mambo yanayotarajiwa katika droo ya mechi za Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
inayopangwa leo mjini hapa.
Droo la leo linalohusisha timu nane kama kawa kutoka nchi
saba tofauti, linahusisha mabingwa sita wa zamani— wakiwemo Milan, Bayern
Munich, Benfica na Marseille— pamoja na timu iliyowahi kutinga fainali, Chelsea
na wakuzuka APOEL ya Cyprus .
Barcelona na Madrid, na wakali wao wa mabao Lionel Messi na
Cristiano Ronaldo, watakuwa wapinzani wa kuogopewa ile mbaya hasa kufuatia
kauli ya rais wa UEFA, Michel Platini kwamba timu hizo za Hispania zikikutana
katika fainali itakuwa hatari tupu “bonge la fainali.”
Barcelona ilitwaa taji la nne la Ligi ya Mabingwa msimu
uliopita, baada ya kuitoa Madrid katika
Nusu Fainali ambayo ilishuhudiwa kocha wa Madrid, Mourinho akifungiwa kuhusika
katika mchezo wa marudiano kwa utovu wa nidhamu.
Bado, mabingwa mara tisa wa michuano hiyo, Madrid wameimarika
mno katika msimu huu wa pili chini ya kocha huyo Mreno, ambaye anaweza kuibuka
kocha wa kwanza kutwaa mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa akiwa na klabu tatu
tofauti.
Mourinho alitwaa taji hilo akiwa na FC Porto mwaka 2004 na
Inter Milan 2010, lakini alishindwa kumpa taji hilo mmiliki wa Chelsea, Roman
Abramovich katika miaka yake mitatu ya kupiga kazi London.
Chini ya Mourinho, Inter iliifunga Chelsea katika hatua ya 16
bora miaka miwili iliyopita na safari yake ya kuelekea taji hilo inaweza
kumpeleka tena Magharibi mwa London baada ya wakongwe Didier Drogba, John Terry
na Frank Lampard kufanya kazi ya ziada na kuitoa timu matata Napoli juzi.
“Watu hawawezi kuelewa kiasi gani naipenda Chelsea na
ninafahamu ikiwa nitakutana nao kwenye Robo Fainali, watakuwa wapinzani wakubwa,”
alisema Mourinho juzi baada ya Madrid kushinda kwa jumla ya mabao 5-2 dhidi ya
CSKA Moscow. “Ningependa kucheza nao katika fainali.”
Ushindi wa Chelsea unaihakikishia England kuendeleza rekodi
yake ya kuwa nchi pekee iliyofululiza kufika Robo Fainali tangu kuanzishwa kwa
michuano hiyo mwaka 1997.
Mechi za kwanza zitachezwa Machi 27 na 28, wakati marudiano
yatakuwa Aprili 3 na 4.
UEFA pia itataja leo tarehe za Nusu Fainali wakati fainali
inafahamika itapigwa Mei 19 mjini Munich.
Bayern inawania kuwa timu ya kwanza kuwania taji katika ardhi
ya nyumbani tangu AS Roma ifungwe mwaka 1984 kwenye Uwanja wa Olympic dhidi ya
Liverpool. Madrid pekee (1957) na Inter (1965) zilitwaa ubingwa huo wa Ulaya
katika viwanja vyao.
Pamoja na kwamba mwaka huu Ligi ya Mabingwa imekuwa
haitabiriki, lakini Robo Fainali imetengeneza uwiano wa nguvu.
Timu sita zimetwaa mataji 27 katika miaka 56, wakati Chelsea ilikaribia
kutwaa katika fainali ya mwaka 2008 kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Manchester
United.
Barcelona inaweza kuibuka klabu ya kwanza kutetea taji hilo
ndani ya miaka 20, tangu enzi za michuano ya zamani, haijaingizwa kwenye mfumo
huu mpya unaotumika sasa.
Marseille walikuwa mabingwa wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa wakiifunga
Milan 1-0 katika fainali mwaka 1993 kwenye Uwanja wa Olimpiki, Munich.
Wafaransa hao sasa wanatinga Robo Fainali kwa mara ya kwanza
tangu wakati huo.
Droo la leo, linaweza pia kuzikutanisha timu zilizokutana kwenye
fainali mwaka 1994, wakati Milan ilipoifunga Barcelona mabao 4-0 mjini Athens.
APOEL wanataka kuleta hadithi ya Cinderella kwa kuwa timu ya
kwanza ya Cyprus kufika hatua hii, kwa bajeti yao ya mishahara timu nzima ya
dola za Kimarekani Milioni 13, ambayo haifikii mshahara anaopewa Mourinho pekee
pale Madrid.
Klabu hiyo kutoka jiji la Nicosia imefuzu Robo Fainali licha
ya kufunga mabao machache tu, saba kama Barcelona na Bayern walivyofanya kwenye
mechi zao moja moja zilizopita.
APOEL imepigwa bao na Messi, ambaye rekodi yake ya mabao
katika mashindano ya msimu huu ni 12 yakiwemo matano aliyofunga kwenye ushindi
wa 7-1 dhidi ya Bayer Leverkusen wiki iliyopita na Mario Gomez, aliyefunga
manne kwenye ushindi wa 7-0 dhidi ya FC Basel Jumanne na kufikisha mabao 10.
0 comments:
Post a Comment