Tostao |
MWANASOKA wa zamani wa kimataifa wa Brazil, Tostao amesema
kwamba mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi ni mzuri kuliko Diego Maradona alivyokuwa,
lakini amesema kwamba kijana huyo wa miaka 24 hajafikia ubora wa Pele.
Messi alitwaa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia wa FIFA kwa
mara ya tatu mapema mwaka huu, na wengi wanamchukulia mchezaji bora daima
duniani.Pamoja na hayo, Tostao mwenye umri wa miaka 65 anafikiri kwamba mshambuliaji huyo wa Barca bado ana hatua ndefu kufikiwa levo za Pele.
"Hata bila ya kuangalia idadi ya mataji aliyotwaa na mabao aliyofunga, sina shaka kabisa kwamba yeye [Messi] tayari ni bora zaidi ya Maradona," alisema Tostao.
"Wengi hawawezi kukubali kwa sababu hajashinda Kombe la Dunia au kufunga bao la ajabu kwenye mechi kubwa katika Kombe la Dunia, lakini kwa kiwango chake cha kisasa, yuko nyuma ya Pele pekee kwa mtazamo wangu.
"Pele alikuwa kamili haswa na alikuwa ana vitu ambavyo Messi anakosa. Alifunga mabao mengi kwa kichwa kwa mfano, na alijua kuutumia mwili wake,”alisema.
Messi tayari amefunga mabao 35 katika mechi 28 za La Liga msimu huu.
0 comments:
Post a Comment