HATIMAYE kiu imejibu, baada ya miezi kadhaa ya ukame wa mabao,
Fernando Torres ameonyesha thamani yake ya kusajiliwa kwa pauni Milioni 50.
Mabao mawili ya Torres kipindi cha pili dhidi ya Leicester
City kwenye Kombe la FA Jumapili, yalimrejeshea furaha mshambuliaji huyo kinda.
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 27, pia alitoa pasi za mabao
mawili katika mechi ambayo alionyesha uwezo mkubwa, Chelsea ikishinda 5-2.
Chelsea ikiwa imetinga fainali ya Kombe la FA na Robo
Fainali ya Ligi ya Mabingwa, mechi 17 zilizobaki chini ya kocha wa muda, Roberto
Di Matteo, zitatoa jibu kama kweli Torres amerudi kwenye anga za kutikisa
nyavu, au alibahatisha tu.
Mtihani wa kwanza wa Torres ni kwenye ni mechi ya Jumatano na
Manchester City kwenye Uwanja wa Etihad, kabla ya kwenda katika mitihani
mingine na Tottenham, Uwanja wa Stamford Bridge. Na zaidi anakabiliwa na
upinzani wa namba na Didier Drogba.
0 comments:
Post a Comment