// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TIMU LA MARADONA LAITISHA CHELSEA ULAYA, LAPIGA MTU SITA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TIMU LA MARADONA LAITISHA CHELSEA ULAYA, LAPIGA MTU SITA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Saturday, March 10, 2012

    TIMU LA MARADONA LAITISHA CHELSEA ULAYA, LAPIGA MTU SITA


    Ezequiel Lavezzi, mtu hatari aliyewafunga Chelsea mechi ya kwanza na jana katupia tena.

    CHELSEA mmeipata hiyo? Napoli, timu ya zamani ya Diego Armando Maradona imepiga mtu goli sita. Ikielekea kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Chelsea katika hatua ya 16 Bora, Napoli imeichapa Cagliari mabao 6-3 jana, huo ukiwa ushindi wake wa sita mfululizo kwenye mashindano yote.
    Wakati huo huo, Inter Milan imeipiga Chievo Verona 2-0 kwa mabao ya dakika za lala salama ya Walter Samuel na Diego Milito na kumaliza nuksi la kutoshinda ndani ya mechi nane mfululizo.
    Marek Hamsik, Paolo Cannavaro, Ezequiel Lavezzi, Walter Gargano na Christian Maggio kila aliifungia bao Napoli, ambayo pia ilinufaika na bao la wapinzani wao kujifunga, kupitia kwa Davide Astori.
    Mshambuliaji wa Argentina, Joaquin Larrivey aliifungia mabao matatu peke yake Cagliari.
    Napoli sasa inashikana na Udinese katika nafasi ya nne, wakizidiwa point inane na vinara wa Serie A, AC Milan, ambao leo wanaikaribisha Lecce. Inter imepanda hadi nafasi ya sita ikizidiwa pointi 14.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TIMU LA MARADONA LAITISHA CHELSEA ULAYA, LAPIGA MTU SITA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top