UONGOZI wa klabu ya Ruvu Shooting umesema unasikitishwa na
kitendo cha Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kuwapa hundi 'feki' na kukaa kimya
kuwalipa Sh 5 milioni wanazodai tangu mwaka 2010.
Akizungumza kwa simu kutoka Ruvu mkoani Pwani jana, meneja
wa Ruvu Shooting, Narcis Ndunguru alisema kuwa fedha wanazodai ni zile
zinazotolewa na wadhamini kwa klabu zote zinazoshiriki Ligi Kuu kwaajili ya kugharimia usafiri na
malazi.
"Ndugu hapa tunapoongea tunaidai TFF sh5,447,500 za
usafiri na malazi tangu mwaka 2010 wamekuwa wakitupiga danadaga tu.
"Tunashangaa kwanini hawatulipi wakati ni haki yetu,
lakini kama wadhamini wanatoa hela zinaenda wapi?.,"alisema Ndunguru.
Alifafanua zaidi kwa kusema kuwa awali Novemba 3, 2011,TFF
iliikabidhi klabu hiyo hundi yenye namba 981944, lakini chakusikitisha ni
kwamba walipoipeleka benki waliambiwa ni feki na ndipo walichukua jukumu la
kuirudisha ingawa alidai tangu wakati
shirikisho hilo halijawalipwa zaidi ya kuwazungushwa.
"Hawajamaa wametuzungusha sana, kila siku njoo kesho
njoo kesho, kifupi ni kwamba awaliTFF ilipotupa hundi hewa, hii ilibainika baada ya kuipeleka benki Novemba 18, 2010,
kinachoshangaza inakuaje tupewe hundi feki? na kama akaunti yao ilikuwa haina
hela kwanini waliitoa,ili ni kosa kubwa,"alisema Ndunguru.
Aliongeza kuwa Agosti 27 mwaka jana waliiandikia barua TFF
kuwakumbusha juu ya deni lao ambapo waliahidiwa kulipwa ingawa alidai ahadi hiyo pia haijatekelezeka
mpaka sasa.
"Baada ya ukimya wao tuliwandikia barua lakini
waendeleleza sera ile ile ya tutawalipa sasa mpaka lini wakati na sisi
tunamipango yetu?.,"alihoji Ndunguru
Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alipotafutwa ili aweze
kujibu malalamiko hayo ya Ruvu Shooting alisema wenye nafasi nzuri ya
kulizungumzia ni kamati ya ligi ingawa jitihada za kumsaka mwenyekiti wa kamati
hiyo Wallace Karia ili atoe ufafanuzi wa suala hilo ziligonga mwamba huku simu
yake ya mkononi ikiita bila majibu.
0 comments:
Post a Comment