Tevez akitupia |
MSHAMBULIAJI Carlos Tevez amekata weight ile mbaya tangu
arudi kazini Manchester City mwezi uliopita na sasa yuko tayari kufanya mamboz
kuipuiga tafu timu yake katika vita ya ubingwa wa Ligi Kuu.
Mshambuliaji huyo wa Kiargentina aliifungia bao timu yake
katika akiichezea kikosi cha wachezaji wa akiba dhidi ya Bolton usiku wa jana,
hiyo ikiwa mechi ya kwanza kuonekana hadharani akiwa na jezi ya City baada ya
zaidi ya miezi mitano.
Katika dakika 66 alizocheza kwenye Uwanja wa Hyde, akifuatiliwa
na Kocha Msaidizi wa City, Brian Kidd Ofisa Utawala, Brian Marwood, Tevez alionekana
mwepesi zaidi ya alivyokuwa mechi iliyochezwa milango imefungwa dhidi ya
Preston wiki iliyopita.
Na City iko tayari kumpokea tena baada ya mavitu adimu
aliyofanya jana.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, alirejea kwenye
klabhu hiyo akiwa hayuko fiti na baada ya kuimarika anaweza kucheza mechi dhidi
ya Chelsea, Machi 19.
Tevez, ambaye alikaribishwa na mashabiki wapatao 1000 wa City,
anatarajiwa kusafiri na kikosi hicho cha wachezaji wa akiba katika mchezo
mwingine wa kirafiki wiki ijayo dhidi ya NEC Nijmegen nchini Uholanzi.
Tevez alikorofishana na kocha wa City, Roberto Mancini baada
ya kugoma kuingia kucheza dakika za lala salama mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi
ya Bayern Munich, Septemba mwaka jana.
Lakini baadaye aliomba radhi kwa Mtaliano na sasa
anatarajiwa kurejea dimbani kwenye kikosi cha vinara hao wa Ligi Kuu muda si mrefu.
0 comments:
Post a Comment