SHIRIKISHO la soka Tanzania (TFF) limesema adhabu walizopewa
wachezaji wa klabu ya soka ya Yanga ni sahihi kwani kumpiga mwamuzi ni utovu wa
nidhamu.
Hatua hiyo inafuatia Yanga kulalamikia adhabu ya vifungo na
faini waliyopewa wachezaji wake watano kutokana na kumpiga mwamuzi Israel
Nkongo mmwishoni mwa wiki iliyopita wakati Yanga ilipocheza na Azam Fc katika
mechi ya Ligi Kuu Bara kwewnye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam .
Rais wa TFF Leodger
Tenga alisema wachezaji hao waliadhibiwa kwa mujibu wa sheria na Kanuni za soka
na mchezaji yoyote atakayeonyesha vitendo vya utovu wa nidhamu ataadhibiwa kwa
mujibu wa kanuni.
“Wachezaji kumpiga mwamuzi si tu kinyume cha sheria ni utovu
wa nidhamu…haya mambo yalikuwa zamani lakini kwa sasa mambo hayo yanatakiwa
kufanywa katika mechi za mchangani lakini si kwa wachezaji ambao tunateghemea
siku moja wakacheze soka la kulipwa nje ya nchi,”Alisema Tenga.
Kama hiyo haitoshi, Tenga alishangazwa na kitendo cha wazee
wa klabu ya Yanga kutoa malalamiko yao na kutishia mamboi kadhaa kuhusiana na
adhabu waliuzopewa wachezaji wa timu hiyo na kusema kuwa walipaswa kukemea
vitendo vya utovu wa nidhamu kwani msimamo walioutoa inaonyesha wanaunga mkono
wachezaji wa Yanga.
“Utu Uzima Dawa si Sumu…haiwezekani wachezaji watende vile
halafu mzee asikemee kwani kwa kufanya hivyo inaondoa kauli mbiu ya Yanga DAIMA
MBELE NYUMA MWIKO…lakini hilo
halipo kwao,”Aliongeza Tenga.
Katika hatua nyinmgine, Tenga amesema kuanzia sasa uharibifu
wowote utakaotokea kwenye uwanja wa Taifa klabu husika italazimika kulipa
gharama ya shilinmgi milioni 10 iliyoelekezwa na Serikali.
Tenga alisema Serikali ina haki ya kutoza faini hiyo
kutokana na Watanzania kushindwa kuonyesha ustaarabu wa kuuthamini uwanja huo
uliojengwa na Serikali na badala yake wamekuwa wakiuharibu kutokana na vurugu
zisizo na maana ambazo hufanywa na mashabiki wa baadhi ya vilabu.
“Ni sawa kwa Serikali kutangaza faini kwa uharibifu
utakaotokea kwenye Uwanja wa Taifa lakini pia ifike mahali viongozi wa vilabu
husika kuwaelimisha wanachama na wapenzi wao kuacha kufanya mambo yasiyo ya
kistaarabu ndani ya uwanja kwani ni vigumu kwa TFF pekee kusimamia suala la
ulinzi ama uangalizi wa uwanja,”alisema Tenga.
Aidha, Tenga aliongeza mpira ni burudani na furaha hivyo
mambo ya kihuni yanayofanywa na baadhi ya mashabiki hayaendani na lengo la
michezo na kwa mwendo huo itafikia wakati makampuni yataacha kudhamini mchezo
huo na matokeo yake kuendelea kurudisha nyuma kiwango cha mchezo huo.
0 comments:
Post a Comment