MWANASOKA wa zamani wa Brazil, Ricardo Teixeira, amejiuzulu
Ujumbe wa Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Teixeira amejiuzulu kwenye nafasi ambayo amekuwa akiishikilia
tangu mwaka 1994 akiwasilisha barua kwa Shirikisho la Soka Amerika Kusini jana.
Mbrazil huyo alisema anajitoa kwenye Kamati hiyo kwa sababu
zake binafsi. Tangazao linakuja takriban wiki moja tangu Teixeira aaachie ngazi
urais wa Shirikisho la Soka Brazil na
Kamati ya Maandalizi ya Kombe la Dunia 2014.
Miaka yake 23 ya kuitumikia soka yaBrazil ilikuwa ya
mafanikio, lakini pia tuhuma mbalimbali za uadilifu ziko nyuma yake.
0 comments:
Post a Comment