// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); TAARIFA MUHIMU KUHUSU KLABU ZOTE LIGI KUU ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE TAARIFA MUHIMU KUHUSU KLABU ZOTE LIGI KUU ENGLAND - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 15, 2012

    TAARIFA MUHIMU KUHUSU KLABU ZOTE LIGI KUU ENGLAND

    ARSENAL:



    KOCHA: Arsene Wenger (tangu 30/09/1996)


    MECHI YA MWISHO: Walishinda 2-1 nyumbani dhidi ya Newcastle, Machi 12


    REKODI: 16-8-4


    MFULULIZO: Kushinda mechi 5


    MECHI IJAYO: Ugenini na Everton, Machi 21


    Mikel Arteta amesema hakuna sababu ya mashabiki wa Everton kumzomea atakaporejea Goodison Park wiki ijayo, licha ya kuhamia kwake Arsenal. Kiungo huyo wa Gunners, Arteta alihitimisha miaka sita na nusu ya kuitumikia Evertonmsimu huu alipoomba kuhama. Alisema:: “Hakika siwezi kusubiri kwenda huko, na ninatumasi nitapata mapokezi mazuri, kwa sababu nimejitolea kwa kila kitu Everton wakati nilipokuwa naon na ninaipenda klabu hiyo. Kila mtu alikuwa anafurahi na mimi na pamoja na kuwa nimeondoka, natumai watu wanaelewa. Hakuna sababu kwa yeyote kati yetu kutomfurahia mwenzake.”






    ASTON VILLA:


    KOCHA: Alex McLeish (tangu 17/06/2011)


    MECHI YA MWISHO: Walishinda 1-0 nyumbani dhidi ya Fulham, Machi 10


    REKODI: 7-9-12


    MFULULIZO: Kushinda mechi 1


    MECHI IJAYO: Nyumbani na Bolton, Machi 20


    Mshambuliaji wa Aston Villa, Gabriel Agbonlahor amefurahishwa na Andreas Weimann kwa kuifungia baio timu hiyo kwenye Ligi Kuu. Nyota huyo wa Austrian mwenye umri wa miaka 20 alifunga bao dakika za lala salama dhidi ya Fulham. Agbonlahor alisema: “Amekuwa akifungia kwa timu ya wachezaaji wa akiba na amefunga hat-tricks kadhaa hivi karibuni. Ni njambo la kujivunia kwao kuna vipaji ambavyo vinaibuka kusaidia timu.”alisema.






    BLACKBURN


    KOCHA: Steve Kean (Tangu 17/12/2010)


    MECHI YA MWISHO: Walishinda 2-0 dhidi ya Wolverhampton, Machi 10


    REKODI: 6-15-7


    MFULULIZO: Kushinda mechi 1


    MECHI IJAYO: Nyumbani na Sunderland, Machi 20


    KOCHA wa Blackburn, Steve Kean ana matumaini Junior Hoilett atabakia kwenye klabu hiyo na kuendelea kuwa tegemeo kwenye kikosi cha Rovers kwa mwaka ujao. Hoilett aliifungia mabao yote Rovers katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Wolves wiki iliyopita, hivyo kumfanya Kean azungumzie nia yake ya kumbakisha kikosini nyota huyo wa mabao wa Canada. Kean alisema: “Tunatajkiwa kufanya kitu Fulani kuhusu Junior. Tuna matumaini. Amekuwa kwenye akademi tangu ana umri wa miaka 13, tumeona maendeleo yake na tuna wachezaji wengi chipukizi.”










    CHELSEA:


    KOCHA: Roberto Di Matteo (tangu 05/03/2012)


    MECHI YA MWISHO: Walishinda 1-0 nyumbani na Stoke, Machi 10


    REKODI: 14-7-7


    MFULULIZO: Kushinda mechi 1


    MECHI IJAYO: Ugenini na Man City, Machi 21


    ULAYA: Wametinga Robo Fainali Ligi ya Mabingwa






    Kaimu Kocha Mkuu wa Chelsea, Roberto Di Matteo anakabiliwa na mtihamim mzito sasa akiifuata Manchester City, lakini ameiwezesha timu kushinda mechi tatu tangu arithi mikoba ya aliyekuwa bosi wake, Andre Villas-Boas. Ameshida mechi ya Kombe la FA dhidi ya Birmingham, ya ligi nyumbani na Stoke kabla ya kuitandika Napoli ya Italia 4-1 na kuingia nane Bora ya Ligin ya Mabingwa Ulaya. Kufuatia ushindi dhidi ya Napoli, Di Matteo alisema: “Nimekuwa na siku za usiku mzuri, natakiwa kusema, lakini nafikiri itaingia kwenye historia ya klabu.”










    BOLTON:


    KOCHA: Owen Coyle (tangu 08/01/2010)


    MECHI YA MWISHO: Walishinda 2-1 nyumbani dhidi ya QPR, Machi 10


    REKODI: 7-19-2


    MFULULIZO: Kushinda mechi moja


    MECHI IJAYO: Ugenini na Aston Villa, Machi 20


    Beki wa Bolton, Marcos Alonso yuko tayari kupigania kurejea kwenye kikosi cha kwanza baada ya kukosa sehemu kubwa ya msimu kutokana na kuwa majeruhi. TMspanyola huyo amekuwa nje kwa takriban miezi mitatu kwa sababu ya maumivu ya mguu aliyopata Desemba kwenye mechi na Blackburn. Alisema: “Kwa ujumla najisikia vizuri haswa. Tumebakiza mechi 10 za Ligi Kuu,kila mechi kwetu ni kama fainali ya kuwania Kombe kwa sababu tunataka kushinda kila mechi kati ya hizo. Nahisi mwenye kujiamini tutapanda kwenyen msimamo wa ligi na kuhakikisha tunabaki Ligi Kuu.”














    FULHAM:


    KOCHA: Martin Jol (since 07/06/2011)


    MECHI YA MWISHO: Walifungwa 1-0 na Aston Villa, Machi 10


    REKODI: 9-10-9


    Mfululizo: Kuifungwa mechi 1


    MECHI IJAYO: Nyumbani na Swansea, Machi 17


    Aaron Hughes anaamini itaimarika na itapigana hadi dajkika ya mwisho ya msimu. Hughes,ambnaye anakutana na Swansea, alisema: “Itakuwa ngumu sana, kwa sababu kuna timu nyingi zimetuzunguka sasa zote zina pointi kama zetu. Kila wiki labda labda kila mmmoja atamruka mwenzake, kasha wiki inayofuata labda watashuka. Nafikiri kama tutaendelea kujikongoja hivi hivi kama tulivyofanhya, kwa kushinda mechi mbili ya mechi zetu tatu, hatuwezi kupoteza, kasha tutamaliza katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi.”










    EVERTON:


    KOCHA: David Moyes (tangu 15/03/2002)


    MECHI ILIYOPITA: Walifingwa 3-0 na Liverpool, Machi 13


    REKODI: 10-11-7


    MFULULIZO: Kufungwa mechi 1


    MECHI IJAYO: Nyumbani na Arsenal, Machi 21


    Beki wa Everton, Phil Jagielka amesema kipigo walichiopewa na Liverpool katika mechi ya 217 ya wapinzani wa jadi wa Merseyside kimezalisha presha kuelekea mechi yao ijayo na Sunderland Jumamosi Robo Fainali Kombe la FA. “Vijana wamekuwa wakifanya vizuri haswa na ninaamini kipigo hiki kitawashusha morali kuelekea mwishoni mwa wiki na wakati tunatakiwa kuendelea na mwendo mzuri tuliokuwa nao,” alisema Jagielka. “Lakini baada ya matokeo, imeleta presha zaidi kwenye Kombe la FA, kwa sababu 3-0 si nzuri sana.










    LIVERPOOL:


    KOCHA: Kenny Dalglish (since 08/01/2011)


    MECHI YA MWISHO: walishinda 3-0 nyumbani dhidi ya Everton, Machi 13


    REKODI: 11-8-9


    MFULULIZO: kushinda mechi moja


    MECHI IJAYO: Ugenini na QPR, Machi 21


    NAHODHA wa Liverpool, Steven Gerrard hajakata tama kumaliza msimu wa Ligi ndani ya nafasi za nne za juu, ili kukata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao. Pointi 10 zinaitenganisha Liverpool na Arsenal inayoshika nafasi ya nne zikiwa zimebaki mechi 10 msimu wa ligi kufungwa, lakini Gerrard alisema: “Ni mlima wa kupanda, lakini Liverpool haiwezi kusalimu amri. Tunahitaji kushinda mechi nyingi kadiri tuwezavyo ili tuone itatuweka wapi, lakini hatuwezi kuachia ngazi ghadi tuone kabisa haiwezekani.”










    MAN CITY:


    KOCHA: Roberto Mancini (tangu 20/12/2009)


    MECHI YA MWISHO: Walifungwa 1-0 na Swansea, Machi 11


    REKODI: 21-4-3


    MFULULIZO: Kufungwa mechi 1


    MECHI IJAYO: Nyumbani na Chelsea, Machi 21


    ULAYA: Wapo hatua ya 16 ya ya Europa League


    Kiungo Nigel de Jong amesema wachezaji wote wa Manchester City wapo tayari kumkaribisha Carlos Tevez nyumbani kwenye timu hiyo. Mshambuliaji huyo mtata wa Kiargentinahajaichezea City kwa miezi sita, alipotofautiana na kocha, anaweza kuanza kuitumikia tena klabun hiyo wiki ijayo na De Jong amesema: “Kila mmoja yuko tayari. Bado ni mchezaji wa Manchester City, hatujawahi kubisha hilo. Katika kundi na kama mchezaji, hajabadilika. Bnafikiri ubora wake ni faida kwa klabu yeyote, na pia kwetu katika hatua hii.”










    MAN UTD:


    KOCHA: Sir Alex Ferguson (tangu 06/11/1986)


    MECHI YA MWISHO: Walishinda 2-0 nyumbani dhidi ya West Brom, Machi 11


    REKODI: 21-3-4


    MFULULIZO: Kushinda mechi 4


    MECHI IJAYO: Ugenini na Wolverhampton, Machi 18


    ULAYA: Wapo hatua ya 16 Bora ya Europa League


    Sir Alex Ferguson amethibitisha kwamba mchezaji ghali wa Manchester United, Dimitar Berbatov anajiandaa kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu. Mchezaji huyo amekuwa akisota kupata namba kikosi cha kwanza cha United tangu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita, timu hiyo ikifungwa na Barcelona. Ferguson alisema: “Amesema hapati namba kwenye kikosi cha kwanza. Ni ngumu kwangu kumuhakikishia hilo, itamfanya aangalie pengine popote.”










    NORWICH:


    KOCHA: Paul Lambert (tangu 18/08/2009)


    MECHI YA MWISHO: Walitoka 1-1 nyumbani na Wigan, Machi 11


    REKODI: 9-10-9


    MFULULIZO: Sare 1


    MECHI IJAYO: Ugenini na Newcastle, Machi 18


    Norwich imepania kufanya kila inaloweza kuhakikishab Paul Lambert anabakia kwenye klabu hiyo msimu ujao. Ofisa Mtendaji Mkuu, David McNally alisema: “Paul anafurahia hapa. Hii ni klabu yake, anakubalika mbele ya Norwich na kwa Norfolk. Ana matarajioa makubwa. Bado hatujamuangusha – tumeendana na matarajio yake, kutoka nafasi ya 69 hadi ya 12. Tutafanya kila tutakaloweza ili tufanye naye kazi muda mrefu.”






    NEWCASTLE


    KOCHA: Alan Pardew (tangu 09/12/2010)


    MECHI YA MWISHO: Walifungwa 2-1 na Arsenal, Machi 12


    REKODI: 12-8-8


    MFULULIZO: Kufungwa mechi 1


    MECHI IJAYO: Nyumbani na Norwich, Machi 18


    Kiungo wa Newcastle, Hatem Ben Arfa anatarajiwa kuwa kila kitu katika kampeni ya The Magpies kuwania nafasi ya kucheza michuano ya Ulaya. Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 25, aliipa timu ya Alan Pardew matumaini ya ushindi wa pili wa pili mfululizo dhidi ya Arsenal kwa bao lake la dakika ya 14 kabla ya Robin van Persie kusawazisha na Thomas Vermaelen kiufunga la ushindi dakika za majeruhi. Ben Arfa alisema: “Tumebakiza mechi 10 na sasa tunatakiwa kujiandaa kufanya kazi kwa ajili ya kuvuna kitu mwishoni mwa msimu.”










    QPR


    KOCHA: Mark Hughes (tangu 10/01/2012)


    MATOKEO YA MWISHO: Walifungwa 2-1 na Bolton, Machi 10


    REKODI: 5-16-7


    MFULULIZO: Kufungwa 1


    MECHI IJAYO: Nyumbani na Liverpool, Machi 21


    Kocha Msaidizi, Mark Bowen bado anajiamini QPR itanusurika kushuka daraja. Timu hiyo inashika nafasi ya 18 katika Ligi Kuu ambayo ni mbaya kwao, kwani wanaeldeekea kurejea Daraja la kwanza, lakini Bowen alisema: “Tuna mechi 10 za kupigana na klabu nyingine nne, kama timu tunatengeneza nafasi nyingi za kufunga mabao, lakini kufunga imekuwa tabu,”alisema.














    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: TAARIFA MUHIMU KUHUSU KLABU ZOTE LIGI KUU ENGLAND Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top