KLABU ya Swansea City iliweza kujipenyeza katika nafasi ya
nane ya Ligi Kuu ya England, baada ya Gylfi Sigurdsson kuongezea mabao mawili
zaidi ambayo yaliiwezesha timu yake kujihakikishia ushindi ilipocheza na
Fulham, na kupata ushindi wa tatu mfululizo katika mechi ya ligi kuu.
Kiungo huyo wa kati alifunga bao la pili katika kipindi cha
pili, baada ya kuupokea mpira kutoka kwa Wayne Routledge.
Joe Allen alikamilisha utaratibu huo wa kuondoka na ushindi
kutoka Craven Cottage, kupitia mkwaju kutoka yadi 18.
Kinyume na matazamio ya mashabiki wengi, wachezaji wa Fulham
walishindwa kuvuma, kama ilivyotazamiwa, na ngome yao ikiwa ni dhaifu mno.
Swansea, tangu kuishinda Manchester City, imekuwa ni timu ya
nne kupata ushindi katika uwanja wa Fulham msimu huu.
Huo ulikuwa ni ushindi wa nne ugenini msimu huu kwa timu hiyo
ya Wales.
Timu hiyo imewathibitishia wote kwamba itaweza kusalia katika
michuano ya ligi kuu ya Premier.
Huku Kocha Martin Jol akishindwa kuiokoa timu yake, Wigan nao
walijipata katika matatizo katika mechi ya pili ya Jumamosi, kwani wanaendelea
kuwa katika nafasi ya mwisho katika ligi ya msimu huu, baada ya kukosa
kuzitumia vyema nafasi za kufunga mabao, na hatimaye kutoka sare ya 1-1
walipocheza na West Brom.
James McArthur aliiwezesha Wigan kutangulia kufunga katika
kipindi cha pili, lakini Paul Scharner aliiwezesha Albion kusawazisha.
Iwapo Wigan wangelipata ushindi, basi wangelifanikiwa
kujinusuru kuondolewa kutoka ligi kuu, lakini kabisa walishindwa kuzitumia
nafasi zilizojitokeza.
0 comments:
Post a Comment