Ssentongo Mabao |
HAWEZI kuacha kufunga mabao na URA haiwezi kuacha kushinda
katika Ligi Kuu ua Uganda, Bell Super League, japokuwa mechi nyingine tatu
zimeshindikana kufanyika kutokana na wachezaji kugoma wakidai haki zao.
Si mwingine, alikuwa ni mshambuliaji wa zamani waq, Robert
Ssentongo alipoipachikia mabao mawili URA katika ushindi wa 4-1 dhidi ya Bidco.
Wakusanya kodi hao wa Uganda, wamekuwa katika wiki tatu nzuri
mno, kwani pia wamesonga mbele katika Ligi ya Mabingwa.
Mshambuliaji wa The Cranes, Ssentongo aliyefunga mawili pia
katika ushindi wa 4-1 kwenye mechi yao iliyopita ya ligi dhidi ya Fire Masters,
alipiga mabao hayo jana katika dakika za 11 na 12.
Moses Feni alifunga la kwanza timu hiyo ya Alex Isabirye, ambayo
inaendelea kuwa juu ya Bunnamwaya inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 37
dakika ya 22 kabla ya Nyanzi Umari kuifungia Bidcodakika nane baadaye.
Lakini Ssentongo alifunga kabla ya mapumziko na linguine dakika
ya 61. Bao la Hamis Kitagenda dakika
nane kabla ya filimbi ya mwisho lilihitimisha karamu ya mabao ya URA dhidi ya
kikosi cha Richard Makumbi, Bidco ambacho kinaporomoka hadi nafasi ya 11 kwa
pointi zake 20.
0 comments:
Post a Comment