Moeneeb Josephs, Andile Jali, Siphiwe Tshabalala na
Itumeleng Khune.
|
JAMBO la kushangaza zaidi kwenye kikosi cha kwanza cha Kaizer
Chiefs kuelekea Soweto Derby dhidi ya wapinzani wao, Orlando Pirates ilikuwa ni
kukosekana kwa kiungo wao babu kubwa Tinashe Nengomasha.
Lakini The Glamour Boys wanapata ahueni mpya kwa kurejea kwa
kiungo mshambuliaji, Siphiwe Tshabalala,
ingawa uamuzi wa kumtema kikosini Nengomasha unaweza kuigharimu Pirates hususan
katika utengenezaji mashambulizi.
Orlando Pirates na Kaizer Chiefs watafufua upinzani wao
maarufu watakapomenyana katika mechi ya Absa Premiership kwenye Uwanja wa FNB jioni
ya leo.
Pirates wanatoka kwenye kipigo cha 3-0 ugenini mbele ya to
Santos katikati ya wiki, kipigo ambacho kilizima wimbi lao la ushindi kwenye
mechi nne mfululizo.
Timu hiyo ya Soweto ina rekodi ya kutofungwa nyumbani msimu
huu, ikiw aimeshinda mechi saba imetoa sare tatu katika mechi 10.
Wamefungwa bao moja tu nyumbani msimu.
The Buccaneers wanashika nafasi ya tatu katika Absa
Premiership wakiwa na pointi 33 katika mechi 19.
Chiefs hawajafungwa katika mechi zao sita zilizopita za ligi,
licha ya kwamba walibanwa kwa sare ya 1-1 na Bidvest Wits katika mechi yao ya
mwisho ya ugenini.
VIKOSI:
Kaizer Chiefs: I Khune,
Tau, Ritchie, Zvasiya, Isaacs, Katsande, Masango, Baloyi, Lebese, Tshabalala,
Parker. Subs: Bartman, Majoro, Lawler, L. Khune, Jambo, Nale, Dladla.
Orlando Pirates:
Josephs, Nzunga, Matlaba, Mahamutsa, Sangweni, Jali, Segolela, Manyisa, Klate,
Mabena, McCarthy. Subs: Meyiwa, Ntshumayelo, Cloete, Rantie, Chansa, Mayambela,
Mabalane.
Refa: Robert Sithole
0 comments:
Post a Comment