// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SOMA BALAA HILI LA COLOMBIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SOMA BALAA HILI LA COLOMBIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Thursday, March 15, 2012

    SOMA BALAA HILI LA COLOMBIA


    BOGOTA, Colombia
    POLISI imesema inashikilia watu 135 baada ya vurugu zilizosababisha watu 11 kujeruhiwa nchini Colombia.
    Mamlaka imesema leo kwamba watu watatu walikuwa wana hali mbaya sana baada ya mashabiki wa Amerika na Deportivo Cali kugombana kabla na wakati wa mchezo katika vurugu zilizoendelea hata baada ya mechi hiyo ya Copa Colombia jana mjini Cali.
    Mashabiki hao walizipiga licha ya kwamba pande zote mbili za mashabiki wa timu hiyo zilikubaliana amani kuelekea kwenye mchezo huo.
    Maofisa walisema askari Polisi mmoja alipoteza kidole chake katika mapambano hayo.
    Jumapili iliyopita, mtu alipigwa risasi na kufariki na wengine tisa walijeruhiwa kwa visu, baada ya mashabiki wa wapinzani wa jadi wa Medellin, Atletico Nacional na Independiente kupigana.
    Polisi ilisema watu 315 walikamatwa na kukamata visu zaidi ya 450 wakati huo
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SOMA BALAA HILI LA COLOMBIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top