// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SOKA LA BONGO LAZIDI KUTITIA, TENGA HASARA TUPU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SOKA LA BONGO LAZIDI KUTITIA, TENGA HASARA TUPU - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Friday, March 09, 2012

    SOKA LA BONGO LAZIDI KUTITIA, TENGA HASARA TUPU

    Rais wa TFF, Tenga anayeua soka ya Tanzania kwa uongozi wake mbovu
    TANZANIA imezidi kuporomoka kwenye orodha ya viwango vya ubora wa soka vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) kila mwezi, na sasa imeshuka kwa nafasi mbili kutoka 139 hadi 141.
    Kwa mujibu wa orodha hiyo iliyotolewa jana jijini Zurich, Uswisi, Tanzania inashika nafasi ya 42 kwa Afrika, huku Uganda ikishika nafasi ya 88 duniani na 20 kwa Afrika.
    Kenya imeshika nafasi ya 113 duniani na 31 Afrika, wakati Rwanda ikiwa nafasi ya 105 duniani na 26 Afrika, huku Burundi ikishika nafasi ya 132 duniani na 39 Afrika.
    Kwa maana nyingine, Tanzania inaburuza mkia kwenye orodha hiyo kwa ukanda wa Afrika Mashariki. Bingwa wa dunia na Ulaya, Hispania imeendelea kuongoza katika viwango hivyo, huku nafasi ya pili ikishikwa na Uholanzi na tatu ikienda kwa Ujerumani.
    Uruguay inashika nafasi ya nne, ikifuatiwa na Brazil, ambayo imepanda kwa nafasi mbili baada ya hivi karibuni kuifunga Bosnia-Herzegovina kwa mabao 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki.
    England na Ureno iliyotoka sare ya bila kufungana na Poland, zipo nafasi ya sita na saba. Argentina imejivuta kwa nafasi tatu na kujikita nafasi ya nane, huku Italia ikishika nafasi ya tisa na Croatia nafasi ya 10.
    Ivory Coast inaongoza kwa ubora katika bara la Afrika na duniani ikiwa inashika nafasi ya 15, huku bingwa wa Afrika, Zambia imepanda kwa nafasi mbili, ikiwa nafasi ya nne Afrika na 41 duniani.
    Ifuatayo ni 10 bora kwa upande wa bara la Afrika na kwenye mabano ni nafasi duniani, Ivory Coast (15), Ghana (23), Algeria (35), Zambia (41), Mali (42), Gabon (43), Libya (55), Tunisia (56), Nigeria (57() na Afrika Kusini (60).
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SOKA LA BONGO LAZIDI KUTITIA, TENGA HASARA TUPU Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top