Sir Alex Ferguson |
KOCHA wa Manchester United, Sir Alex Ferguson leo amejibu
mapigo ya wapinzani wao katika mbio za ubingwa wa Ligi Kuu, Manchester City kwamba
mabingwa hao watetezi wanabebwa na marefa.
Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Soka wa Manchester City,
Patrick Vieira alinukuliwa kwa mapana marefu akisema kwamba United na
klabu nyingine kubwa Ulaya zinabebwa na
marefa hasa katika mechi za nyumbani.
Kiungo huyo wa zamani wa Arsenal na City alitolea mfano
United ilivyooepuka adhabu ya penalti, licha ya Michael Carrick kumchezea rafu Danny
Murphy dakika za mwishoni Mashetani Wekundu wakishinda 1-0 dhidi ya Fulham Jumatatu.
Baadaye City ilisema maneno ya Vieira yalikuwa yak wake mwenyewe
– lakini Ferguson hakuona sababu ya kuyapuuza katika maelezo yake leo wakati
mbio za ubingwa zinaelekea kileleni.
Ferguson alisema United pia walitakiwa kupata penalti Jumatatu
dhidi ya Fulham, akisema kwamba maamuzi kama hayo hata na wao wanakutana nayo.
"Nafikiri tulitakiwa kupewa penalti Jumatatu usiku,"
alisema Ferguson.
"Lakini usitarajie kupata kama hiyo, wakati mchezaji wa
pembeni anatia krosi na mchezaji anaunawa mpira kwa bahati mbaya. Tungepeta penalti,
lakini hatukutarajia, niwe mkweli kwao,”alisema.
"Nafikiria hilo kulingana na nafasi ya refa, naweza
kuona kwa nini refa hakutoa penalti wakati Danny Murphy alipoangushwea kwenye
eneo letu la hatari, kwa sababu mpira ulikuwa unaelekea pembeni wakati Michael
Carrick anakwenda kumkabili.
"Kulingana na nafasi, haikuwa sahihi, lakini yalikuwa
malalamiko mazuri.
"Lakini pia City wangepata penalti dhidi ya Stoke, kama
kila mtu alivyoona, wakati Gareth Barry alipomkabili Glenn Whelan. Hivyo hayo
unakutana nayo hapa na kule.
"Tulikumbana na uamuzi wa utata Old Trafford, wakati
Newcastle walipopewa penalti. Tottenham wanaweza kulalamika hivyo pia wakati
Balotelli alipoachwa uwanjani hadi akafunga bao la ushindi katika ushindi wa City
3-2, ingawa alistahili kutolewa kwa kadi nyekundu..
Ferguson pia alitoa wasiwasi kwamba kipa Anders Lidegaard hatacheza
tena msimu huu baada ya kuumia mazoezini, akisema kwamba anaendelea vizuri na
maumivu yake ya kifundo cha mguu.
Kocha huyo wa United pia amempata tena beki Rio Ferdinand aliyekuwa
majeruhi kuelekea mechi ya Jumatatu ugenini dhidi ya Blackburn, na sasa majeruhi
wake pekee ni Nani.
0 comments:
Post a Comment