// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA WAWAHI WENYEWE POLISI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA WAWAHI WENYEWE POLISI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 12, 2012

    SIMBA WAWAHI WENYEWE POLISI


    Tegemeo la mabao la Simba, Emanuel Okwi jana alitoka kapa mbele ya Toto, vipi Dodoma ataipendezesha Simba?

    BAADA ya kupunguzwa kasi na Toto Africa ya Mwanza jana, Simba inatarajiwa kuendeleza mbio zake za ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kwa kumenyana na Polisi Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri keshokutwa.
    Simba iliyotoka 0-0 katika mchezo mwingine wa wa Ligi Kuu juzi, imeondoka leo Dar es Salaam kwenda Dodoma.
    Jana,Simba iliingia uwanjani ikiwa na matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo na kuzidi kuongeza pengo la pointi na mtani wake Yanga, ambayo juzi ilifungwa mabao 3-1 na
    Azam, lakini ilijikuta ikidhibitiwa na kushindwa kuzifumania nyavu za wapinzani wao.
    Washambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi, Haruna Moshi na Felix Sunzu kwa nyakati tofauti waliingia kwenye eneo la hatari la Toto African lakini umaliziaji ulikuwa butu.
    Dakika ya 13 Patrick Mafisango nusura aipatie bao Toto, lakini alishindwa kuunganisha vyema kutokana na krosi ya beki Nassoro Said Masoud, dakika nne baadaye Toto ilijibu lakini kichwa cha Labani Kambole kilipaa juu ya lango.
    Okwi aliwatoka mabeki wa Toto dakika ya 21, lakini shuti lake liliwagonga mabeki na kuokolewa, kisha dakika ya 28 kulitokea piga nikupige langoni mwa Toto lakini umaliziaji
    haukuwa mzuri.
    Kipindi hicho cha kwanza, Phabian Ngwase naye alifanikiwa kuingia eneo la Simba la hatari mara kadhaa lakini mashuti yake hayakuwa na macho.
    Kipindi cha pili Simba walionekana kucharuka zaidi kwa kufika langoni mwa wapinzani wao
    mara kadhaa lakini ugonjwa wa kukosa mabao uliendelea kuitesa timu hiyo.
    Mchezaji Ally Ally wa Toto naye kipindi cha pili alipoteza nafasi ya kuipatia timu yake bao kutokana na kutokuwa makini katika umaliziaji.
    Mwamuzi wa mchezo huo, Nathaniel Lazaro alimtoa kwa kadi nyekundu beki Kelvin Yondani wa Simba dakika ya 75, baada ya kumpa kadi ya pili ya njano kutokana na kumdanganya mwamuzi kwa kujiangusha eneo la penaltiy, ambapo awali alishaonywa kwa kadi ya njano.
    Kutokana na matokeo hayo, Simba imerejea kileleni ikiwa na pointi 41 sawa na Azam, lakini yenyewe ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga ikiwa na faida ya mabao 19, wakati Azam iliyokuwa ikiongoza sasa inashika nafasi ya pili kutokana na kuwa na faida ya mabao 18.
    Yanga inashika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 37, ingawa Yanga imezidiwa michezo miwili na Azam, pia imezidiwa mchezo mmoja na Simba.
    Toto bado inashika nafasi ya tatu kutoka mkiani kati ya timu 14 zinazoshiriki ligi hiyo ikiwa na pointi 17.
    Katika mchezo mwingine, Polisi inayocheza Simba Jumatano jana iliifunga Kagera Sugar bao 1-0 katika mfululizo wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Jamhuri, bao pekee la mkongwe Bantu Admin akiunganisha krosi ya Juma Semsue dakika ya 50.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA WAWAHI WENYEWE POLISI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top