// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA NA KAGERA SUGAR KWA UNDANI ZAIDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA NA KAGERA SUGAR KWA UNDANI ZAIDI - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 06, 2012

    SIMBA NA KAGERA SUGAR KWA UNDANI ZAIDI


    Kikosi cha Simba kilichowika Afrika Jumapili, kitaendeleza cheche mbele ya Kagera kesho?

    WAKIWA wenye furaha ya kusonga mbele kwenye Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, Simba SC kesho watashuka dimbani, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kumenyana na Kagera Sugar ya Bukoba katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
    Simba iliitupa nje Kiyovu Sport ya Rwanda Jumapili kwa ushindi wa mabao 2-1 unaofanya jumla ya mabao 3-2, baada ya sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza wiki mbili zilizotangulia mjini Kigali.
    Sasa, Wekundu hao wa Msimbazi wanahamishia hasira zao katika Ligi Kuu, ambayo kama ilivyo England, Manchester United na Manchster City zinakabana koo ile mbaya kuwania taji, nao wanakwidana kisawasawa na wapinzani wao jadi, Yanga katika vita ya mwali.
    Simba ina pointi 37 sawa na mabingwa watetezi, Yanga lakini wao wako juu kwa sababu ya baop moja wanalowazidi wababe wao hao katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu.
    Kocha wea Simba, Mserbia Milovan Curkovick hatarajiwi kufanya mabadiliko makubwa katika kikosi chake hasa ikizingatiwa Jumamosi alishinda mechi ya michuano ya Afrika.
    Juma Kaseja, kama kawaida anatarajiwa kulinda lango, akisaidiwa na mabeki Nassor Masoud ‘Chollo’ kulia, Amir Maftah kushoto na katikati Kelvin Yondan na Juma Nyosso waliosaidiwa na Patrick Mafisango katika kiungo cha ulinzi.
    Mwinyi Kazimoto anasumbuliwa na nyama za paja na yuko shakani kucheza leo, lakini Shomary Kapombe au Jonas Mkude mmoja wao anaweza kuziba pengo lake.
    Uhuru Suleiman anaweza kuanza kulia mbele na kushoto Salum Machaku wakati Mzambia Felix Mumba Sunzu Jr aliyetupia mawili yote nyavuni katika ushindi wa 2-1 dhidi ya Kiyovu Jumamosi atakuwa na Mganda Emanuel Okwi katika safu ya ushambuliaji.
    Sunzu na Okwi walicheza kwa ushirikiano mzuri Jumamosi ambao bila shaka Milovan atapenda uendelee.
    Hata hivyo, Nahodha Haruna Moshi ‘Boban’ ataikosa mechi ya leo, kwa sababu bado anatumikia adhabu kwenye Ligi Kuu.
    Kagera Sugar hawatarajiwi kuwa wanyonge kwa Simba leo, kwani kihisto4ria timu hii kutoka mashamba ya miwa ya Misenyi imekuwa ikimtoa sana nishai Mnyama.
    Mwaka 2005, Kagera Sugar iliifunga Simba 2-1 Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kutwaa Kombe la Tusker, enzi hizo kikosi chake kikiundwa na wakali kama Mrisho Ngassa, Omary Changa, Yussuf Macho, Vincent Barnabas, Shamte Ally, Shijja Mkinna na Paul Kabange.  
    Ukiwauliza Simba ilikuwaje wakakosa ubingwa msimu uliopita, katika moja ya sababu wataitaja na Kagera pia- hivyo hii ni timu yenye historia ya kuwanyima raha wana Msimbazi na hii inamaanisha gemu la leo litakuwa tamu.
    Kocha Msaidizi wa Kagera Sugar, Mrage Kabange, amesema anawahofia sana Okwi na Sunzu katika mchezo wa leo, hasa baada ya kucheza soka adimu Jumapili na kutoa mchango mkubwa Simba ikiitoa Kiyovu.
    “Soka siyo siasa, ukweli ni kwamba Okwi na Sunzu wana viwango vya juu, hivyo nimepanga kikosi changu cha kuwadhibiti, ili wasilisogelee lango letu,” alisema. Kagera Sugar inashika nafasi ya nane, kutokana na pointi zake 24.
    Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana Septemba 18, mwaka jana zilifungana bao 1-1, Uwanja wa Taifa. Mambo yatakuwajen Taifa leo? Twendeni tukaone.

    REKODI YA SIMBA NA KAGERA:
    Septemba 18, 2011
    Kagera Sugar 1-1 Simba
    Machi 29, 2011
    Simba 0-0 Kagera Sugar
    Oktoba 27, 2010
    Kagera Sugar 0-2 Simba
    Februari 3, 2010
    Kagera Sugar 1-1 Simba     
    Septemba 10, 2009
    Simba 2-0 Kagera Sugar
    Aprili 5, 2009
    Kagera Sugar 0-2 Simba 
    Oktoba 14, 2008
    Simba 1-0 Kagera Sugar  
    Aprili 19, 2008
    Kagera Sugar 0-1 Simba
    Oktoba 13, 2007
    Simba 2-1 Kagera Sugar
    Oktoba 18, 2006
    Simba 2-1 Kagera Sugar
    Juni 3, 2006
    Kagera Sugar 1-0 Simba
    (Kagera wakapewa ushindi wa mezani
    2-0, kwa Simba kumchezesha Mussa
    Mgosi akiwa ana kadi tatu za njano)
    Septemba 28, 2005
    Kagera Sugar 0-2 Simba    
    Mei 25, 2005
    Simba 0-1 Kagera Sugar
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA NA KAGERA SUGAR KWA UNDANI ZAIDI Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top