// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SIMBA, KIYOVU ZAINGIZA MILIONI 200 NA UPUUZI, MAMBO YA PRIME TIME HAYO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SIMBA, KIYOVU ZAINGIZA MILIONI 200 NA UPUUZI, MAMBO YA PRIME TIME HAYO - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Tuesday, March 06, 2012

    SIMBA, KIYOVU ZAINGIZA MILIONI 200 NA UPUUZI, MAMBO YA PRIME TIME HAYO


    Felix Sunzu kushoto akishangilia na Patrick Mafisango na Emanuel Okwi

    MECHI ya Kombe la Shirikisho Afrika, kati ya Simba SC na Kiyovu ya Rwanda imeingiza kiasi cha 208,843,000.00, imeelezwa.
    Mechi hiyo iliyosimamiwa na kampuni ya Prime Time Promotions ya Dar es Salaam, ilichezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na SImba ilishinda mabao 2-1, yote yakitiwa kimiani na Felix Sunzu.
    Simba imeingia Raundi ya Pili ya Kombe la Shirikisho kwa ushindi wa jumla wa mabao 3-2, kufuatia sare ya 1-1 kwenye mchezo wa kwanza mjini Kigali.  
    Hata hivyo, mapato hayo hayafui dafu kwa mapato ya mechi ya kwanza ya Raundi ya Kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Zamalek ya Misiri, ambayo iliingiza Sh 286, 695.000,00 wiki tatu zilizopita kwenye Uwanja huo huo.
    Katika mchezo, timu hizo zilitoka sare ya 1-1 Yanga ikitangulipa kupata bao lililofungwa na Hamisi Kiiza na Zamalek kusawzisha kupitia kwa Amr Zaki.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SIMBA, KIYOVU ZAINGIZA MILIONI 200 NA UPUUZI, MAMBO YA PRIME TIME HAYO Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top