// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SHEHATA AMSHUKURU MUNGU, ASEMA YANGA HAWAFAI HATA KWA KULUMANGIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SHEHATA AMSHUKURU MUNGU, ASEMA YANGA HAWAFAI HATA KWA KULUMANGIA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 05, 2012

    SHEHATA AMSHUKURU MUNGU, ASEMA YANGA HAWAFAI HATA KWA KULUMANGIA

    KOCHA wa Zamalek Hassan Shehata, amesema hajaridhishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wa timu hiyo kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Yanga na kuibuka na ushindi wa bao 1-0 Jumamosi.

    “Wachezaji wangu hawakufuata maelekezo yangu kwa sababu walifikiri ingekuwa rahisi,” alisema Shehata.
    “Waliidharau mechi hiyo na walidhani wangeweza kupata ushindi muda wowote.Wachezaji
    wa Yanga walionekana kama wangefunga muda wowote kwa sababu ya uzembe wa wachezaji wangu, ” alisema Shehata.
    Kocha huyo mwenye umri wa miaka 62 alisifu kiwango kilichooneshwa na mshambuliaji -Ahmed Hossam “Mido” ambaye alifunga bao la ushindi kwa timu hiyo na kuiwezesha kuvuka kwa raundi inayofuata.
    “Mido bado ana mengi ya kufanikiwa ndani ya kikosi cha Zamalek kwani huo ulikuwa mchezo
    wake wa kwanza baada ya kukaa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.”
    Kwa upande wake Mido, pia alizungumzia matokeo hayo na kusema mchezo ulikuwa mgumu na kwamba walibahatisha kuibuka na ushindi huo.
    Wakati huohuo, Ofisa Habari wa Yanga, Luios Sendeu alisema jana kuwa timu hiyo ilitarajiwa
    kuwasili leo alfajiri na kwamba masuala mengine yote yatazungumzwa baada ya timu kuwasili Dar es Salaam.
    “Wamesema wakifika watazungumza kuhusiana na matokeo hayo kiufundi na mambo mengine, hivyo tunawasubiri warudi salama,” alisema Sendeu.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SHEHATA AMSHUKURU MUNGU, ASEMA YANGA HAWAFAI HATA KWA KULUMANGIA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top