// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); SERIKALI NAYO YAIADHIBU YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE SERIKALI NAYO YAIADHIBU YANGA - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Wednesday, March 14, 2012

    SERIKALI NAYO YAIADHIBU YANGA


    Geoffrey Bonny wa Yanga mbele na Abdi Kassim wa Azam katika iliyotawaliwa na vurugu baina ya timu hizo 
    SHIRIKISHO Soka Tanzania (TFF) leo limepokea barua kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo juu uharibifu uliofanyika kutokana na vurugu za washabiki wa Yanga kwenye mechi dhidi ya Azam.
    Kwa mujibu wa tathmini ya Serikali, katika vurugu hizo kwenye mechi hiyo ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa Machi 10 mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam jumla ya viti 119 viliharibiwa. Gharama za uharibifu huo ni sh. milioni 5 ambazo Serikali imeagiza zilipwe mara moja.
    Kwa vile washabiki wa Yanga ndiyo waliohusika na vurugu na uharibifu huo, gharama hizo zitabebwa na klabu hiyo ili Serikali iweze kufanya ukarabati haraka.
    TFF inarudia tena kulaani na kukemea vurugu zinazofanywa na washabiki viwanjani na kusababisha usumbufu, uvunjifu wa amani na uharibifu wa vifaa  hasa kutokana na ukweli kuwa mpira wa miguu ni mchezo wa burudani.
    Tunapenda kuwakumbusha washabiki na klabu kuwa vitendo hivyo si vya kistaarabu, hivyo havikubaliki katika mpira wa miguu, na TFF haitasita kuchukua hatua kali kwa wahusika iwapo vitaendelea kutokea viwanjani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: SERIKALI NAYO YAIADHIBU YANGA Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top