KOCHA wa zamani wa Chelsea, Luiz Felipe Scolari amesema kufanya
kazi chini ya mmiliki wa klabu hiyo, Mrusi Roman Abramovich ni sawa na kuingia ‘jehanam’.
Luiz Filipe Scolari ameonya atakayetaka kurithi mikoba ya
Villas-Boas aliyetimuliwa Jumapili, ajue hilo.
Abramovich kwa sasa anamtafuta kocha wa nane wa kudumu tangu
mwaka 2003 baada ya kumtimua Andre Villas-Boas siku ya Jumapili.
"Itakuwa sawa na kuingia kuzimu kwa yeyote
atakayechukua nafasi ya Villas-Boast," alisema Scolari,ambaye aliwahi kuwa
meneja wa Chelsea kwa miezi saba kati ya mwaka 2008-09.
"Kumtimua lilikuwa jambo la ajabu, ingawa si ajabu sana
kwangu kwa sababu ya kile nilichokumbana nacho nilipokuwa katika klabu ile.
0 comments:
Post a Comment