Kaburu kushoto, akiwa na Joseph Kusaga |
MAKAMU Mwenyekiti wa Simba, Geofrey Nyange, amesema mara
baada ya ushindi wa jana dhidi ya ES Setif kwenye Kombe la CAF jijini Dar es
Salaam, timu yake sasa inaelekeza nguvu zake kwenye Ligi Kuu ya Vodacom (VPL).
Akizungumza na wachezaji wa Simba mara baada ya pambano la
jana, Kaburu alisema mechi dhidi ya Setif imepita na ni lazima kila mchezaji na
kiongozi aelekeze nguvu na akili yake katika pambano la Machi 31 dhidi ya
African Lyon ya Dar es Salaam."Wataalamu wanasema mpira ni dakika 90. Zikimalizika hizo maana yake unaangalia nini kilicho mbele yako. Tunashukuru kwamba wachezaji leo mmelinda heshima ya Simba na Tanzania na tunawapongeza sana kwa hilo. Lakini ni lazima tujue bado tuna majukumu mengine," alisema.
Kaburu alisema ni muhimu kwa Simba kushinda katika mchezo huo kwa vile sasa inashiriki Kombe la CAF baada ya kushika mojawapo ya nafasi za juu katika VPL msimu uliopita.
"Tukivurunda kwenye ligi maana yake mwakani hatutaweza kushiriki michuano ya kimataifa jambo ambalo halikubaliki ndani ya Simba. Ndiyo maana nasema ni lazima tuelekeze nguvu zetu huko," alisema.
0 comments:
Post a Comment