Katibu wa TASWA, Amir Mhando katikati ambaye ametoa taarifa za msiba wa Mbega. |
MWANDISHI mwandamizi wa habari za michezo nchini, Samson
Mbega amefariki dunia asubuhi ya leo- kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA).
Kwa mujibu wa rafiki wa karibu wa marehemu, Mawazo Lusonzo
ni kwamba msiba upo nyumbani kwa marehemu, nyuma ya kota za Temeke mwisho eneo
la Pile Bar.
Kwangu, Mbega alikuwa kaka na kiongozi, ambaye alinisaidia
kitaaluma. Alinipokea kwenye viwanja vya michezo mwaka 1997 nikiwa gazaeti la
Mfanyakazi, yeye akiwa Majira. Tulikutana na kufanyua kazi pamoja All Sports
Promotions katika gazeti la Ngurumo za Simba na The Kick.
Mbega alikuwa mpole, daima ni kaka ni kiongozi, hakuwa na
makuu. Ni aina ya watu adimu na kifo chake ni pigo. Huo ni ukweli usiofichika. Mungu
aiweke pema peponi roho ya marehemu. Amin. Endeelea kufuatilia bongostaz kwa
taarifa zaidi za msiba huo.
0 comments:
Post a Comment