Samatta |
KLABU ya TP Mazembe imesema maumivu ya mshambuliaji wake wa
kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta si ya kutisha lakini wamepanga
kumpeleka Afrika Kusini kwa uchunguzi zaidi.
Samatta ambaye ataikosa mechi kali dhidi ya DC Motemba Pembe
Aprili 1, mwaka huu katika Ligi Kuu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC),
aliuamia bega kwenye mechi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Power Dynamos
nchini Zambia.
Siku hiyo, Samatta au ‘Samagoal’ kama wamuitavyo mashabiki
wa TPM alifunga bao timu yake ikitoa sare ya 1-1 na kujiwekea mazingira mazuri
ya kusonga mbele.
Tovuti ya TPM imesema Samatta yuko chini ya uangalizi makini
wa wataalamu wa tiba wa klabu hiyo na amekuwa akiupa mazoezi kidogo mkono wake.
Samatta amekuwa akihudhuria kliniki ya TPM kila asubuhi na
jioni pamoja na kutibiwa, lakini pia akijengwa kisaikolojia.
Mchezaji mwingine wa Mazembe aliyekuwa anasumbuliwa na nyama
kwa wiki mbili, beki Hichani Himonde amepona na ameanza mazoezi.
Samatta ataikosa pia mechi ya marudiano na Power Dynamos Aprili
8, mwaka huu, Stade Kibassa Maliba.
0 comments:
Post a Comment