// Disable text selection (not fully reliable) function disableSelection(element) { element.setAttribute('unselectable', 'on'); element.style.userSelect = 'none'; element.style.MozUserSelect = 'none'; element.style.webkitUserSelect = 'none'; } // Apply to the entire document body document.addEventListener('DOMContentLoaded', function() { disableSelection(document.body); }); ROSICKY ASAINI MKATABA MPYA ARSENAL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE ROSICKY ASAINI MKATABA MPYA ARSENAL - BIN ZUBEIRY SPORTS - ONLINE
  • HABARI MPYA

    Monday, March 12, 2012

    ROSICKY ASAINI MKATABA MPYA ARSENAL


    Rosicky akishangilia moja ya mabao aliyoifungia Gunners

    KIUNGO wa klabu ya soka ya Arsenal, Tomas Rosicky, ambaye pia ni maarufu katika kushambulia, ametia saini mkataba mpya na klabu hiyo.
    Rosicky yumo katika hali nzuri sana msimu huu, na ameweza kuifungia Arsenal mara mbili katika mechi tatu zilizopita.
    Meneja Arsene Wenger amesema: "Siku zote nimevutiwa sana na anavyocheza Tomas na hasa uwezo wake mkubwa, na nimefurahi sana ameamua kuendelea kuichezea klabu".
    Rosicky, mwenye umri wa miaka 31, na ambaye ni nahodha wa timu ya Jamhuri ya Czech, alijiunga na The Gunners mwaka 2006, wakati huo akitoka Borussia Dortmund ya Ujerumani.
    Bado haijafahamika mkataba huo mpya ni wa muda gani.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Item Reviewed: ROSICKY ASAINI MKATABA MPYA ARSENAL Rating: 5 Reviewed By: Mahmoud Bin Zubeiry
    Scroll to Top