Ribery |
NAHODHA wa Bayern Munich, Philipp Lahm amefurahia kuziepuka bunduki
kubwa za Hispania katika droo ya Ligi ya Mabingwa Ulaya iliyopangwa jana– lakini
yeyote kutoka timu hiyo ya Bavaria anahitaji kuelewa kwamba ili kuwajua vizuri wapinzani
waliopangiwa, Olympique Marseille, amuulize Franck Ribery pekee.
Mshambuliaji huyo wa Ufaransa alidumu kwa misimu miwili Stade
Vélodrome, kutoka 2005 hadi 2007, na anaufahamu vema ugumu wanaouelekea Bayern katika
mechi ya kwanza mjini Marseille Machi 28, 2011.
“Hii si rahisi,”alisema Ribery alipozungumza na Uefa.com.
"Kwa Marseille itakuwa kimbembe. Watu
wanapenda soka na mashabiki 60 000 watakuwa dhidi yetu."
Akizungumzia Bayern kupangwa na OM, Lahm aliita "droo
yenye akili ", akisema: "Nilisema itakuwa vema kuwaepuka Barcelona na
Real, ndio maana tunaweza kufurahia."
Bado hakuwa sahihi kuamini mabingwa hao wa mwaka 1993 ni
wepesi licha ya wiki hii kutoka kuwang’oa Inter Milan na waliwapiga nyumbani na
ugenini vinara wa Bundesliga, Borussia Dortmund katika hatua ya makundi.
“Marseille ni hatari. Wameitoa Inter na waliifunga mara
mbili Dortmund,"alisema. "Ni ahueni ndogo kwamba, tunaanzia ugenini."
Kwa Marseille, mechi ya pili Aprili 3 itawarudisha Munich, jiji
ambalo walishinda fainali ya Ligi ya Mabingwa mwaka 1993, katika maskani ya
zamani ya Bayern, Uwanja wa Olympia.
Ndoto za Bayern msimu huu ni kucheza mechi ya mwisho katika
Uwanja wao wa nyumbani bna kocha wa Marseille, Didier Deschamps alisema inaweza
hii "inaweza kuwa ya kuvutia kwa wapinzani wetu" kupangiwa timu ya Ligue
1 katika Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa tangu kampeni ya 1992/93.
“Ni ngumu, wako imara sana,"alisema Deschamps, Nahodha
wa kikosi cha Marseille mwaka 1993. "Kulikuwa kuna klabu mbili za Hispania,
Real na Barcelona, lakini nafikiri kwamba Bayern ni timu inayofuatia ubora wao.
Wana wachezaji wa ngvu na wenye kushambulia sana kama
Ribery, [Arjen] Robben, [Thomas] Muller na [Mario] Gomez. Wana kipa wa
kimataifa, [Manuel] Neuer, [Bastian] Schweinsteiger kwenye kiungo na Lahm na
[OM kinda la Daniel] van Buyten katika beki nne. Ni wagumu sana."
Bayern iliifunga timu nyingine ya Ufaransa, Olympique
Lyonnais nyumbani na ugenini katika Nusu Fainali miaka miwili iliyopita, lakini
Deschamps anaamini wamekusdanya uzoefu mkubwa msimu huu, ikiwemo ushindi dhidi
ya Dortmund.
“Lazima tuamini, vyovyote. Ni kweli tumewafunga Dortmund mara
mbili, hata kama haikuwa rahisi. Wana pointi tano zaidi ya Bayern [kwenye
Bundesliga], lakini Dortmund walijiandaa kwa Ligi ya mabingwa mwaka huu. Bayern
ni hivyo pia. Tutapigana kwa uwezo wetu wote kaa tulivyofanya dhidi ya
Inter."
Japo ni rahisi kutabiri mshindi wa Robo Fainali kati ya Real
Madrid na APOEL, lakini Mwenyekiti wa Bayern, Karl-Heinz Rummenigge amesema si
vema kuangalia mbali zaidi.
"Ni vema kwetu kutofikiria uwezekano wa kukutana na Real
kwenye Nusu Fainali. Lengo letu ni kufika Nusu Fainali, ni wazi, lakini lazima
tupige hatua ya kwanza kabla ya hatua ya pili. Mtazamo wetu kamili unatakiwa
kuwa kwa Marseille."
0 comments:
Post a Comment