Santi Cazorla |
BAO la dakika ya mwisho la Santi Cazorla liliisaidia Malaga kupata
sare ya 1-1 na vinara wa La Liga, Real Madrid jana.
Real imejiongezea pointi moja tu na kuwa 71 ikiwa imebakiza
pointi 11 na sare hiyo inakuja baada ya
kushinda mechi 11 mfululizo.
Sare hiyo inawafanya sasa waongoze ligi kwa pointi nane badala
ya 10 kufuatia Barcelona kuifunga Sevilla 2-0 ugenini Jumamosi.
Karim Benzema aliifungia bao la kuongoza Real dakika ya 35.
Katika mchezo mwingine mapema jana, mshambuliaji Roberto
Soldado alifunga mabao matatu peke yake Valencia ikishinda 3-0 dhidi ya
Athletic Bilbao.
Ikicheza pungufu ya mchezaji mmoja, Real Mallorca iliifunga Atletico
mabao 2-1 nyumbani.
Diego Godin wa Atletico alijifunga dakika ya 47, kabla ya Michael
Pereira kufunga la pili dakika mbili baadaye na ndipo wakampoteza beki Ivan
Ramis aliyeushika mpira dakika ya 53.
Dudu Aouate wa Mallorca aliokoa penalti ya Radamel Falcao, ingawa
mshambuliaji huyo wa Colombia aliuwahi mpira na kutumbukiza nyavuni kuwapatia
wageni bao la kufutia machozi dakika ya 66.
0 comments:
Post a Comment