Ronaldo |
OSASUNA inaweza kumkosa Marc Bertran katika mechi na Real
Madrid leo tangu matatizo yake kwenye mechi iliyopita wakishinda Levante Jumapili
waliyoshinda 2-0.
Kike Sola na Masoud Shojaei wote wapo nje kwa sababu ni
majeruhi, lakini Javad Nekounam anarudi tena baada ya kumaliza adhabu yake ya
mechi moja.
Real Madrid itamkosa Jose Callejon anayeumwa kifundo cha
mguu, Ricardo Carvalho (thigh) na Lassana Diarra (nyama za paja), lakini winga
Angel Di Maria, ambaye amekuwa nje ya Uwanja tangu Februari kwa maumivu, anatarajiwa
kurejea.
Mesut Ozil amemaliza adhabu sambamba na kocha wake Jose
Mourinho, ambaye aliikosa mechi ya ushindi wa 5-1 dhidi ya Real Sociedad baada
ya kutolewa nje kwenye mechi ya sare ya 1-1 na Villarreal.
Raphael Varane anatarajiwa kuendelea kucheza beki ya kati kutokana
na kutokuwepo kwa Pepe, ambaye atakuw aanamalizia mechi yake ya pili ya adhabu.
Vikosi;
OSASUNA: Fernandez, Raitala, Roversio, Flano, Damia, Punal,
Nekounam, Cejudo, Garcia, Lamah na
Nino.
REAL MADRID: Casillas, Arbeloa, Varane, Ramos, Marcelo, Khedira,
Alonso, Ozil, Kaka, Ronaldo, Benzema,
JE WAJUA?
Osasuna wanaoshika nafasi ya sita, hawajafungwa mechi sita
katika La Liga (imeshinda tat, imetoa sare tatu).
The Pamplona wamefungwa mechi mbili tu nyumbani msimu huu – dhidi
ya Racing Santander na Atletico Madrid.
Osasuna, kwa pamoja na Racing, zimetoa sare nyingi zaidi La
Liga msimu huu (13).
Real Madrid imefungwa mechi mbili kati ya ilizokwenda Osasuna.
Ushindi wa mwisho kwa Reyno de Navarra ulikuwa ni Mei 2008.
Cristiano Ronaldo alifunga mawili katika ushindi wa 5-1 dhidi
ya Real Sociedad na kuweka rekodi ya mchezaji wa kwanza kufikisha mabao 100 haraka
zaidi katika historia La Liga (101 ndani ya mechi 92).
0 comments:
Post a Comment